Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo Leo amezindua WIFI ya bure kwa wananchi wa Ilala wote watakaokwenda kununua bidhaa katika jengo la Wafanyabiashara Machinga Complex lililopo Wilayani Ilala watatumia intanet hiyo bure ya Serikali .
Mkuu wa Wilaya Ilala amezindua WIFI hiyo ya bure katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alilolilotoa hivi karibuni akitaka katika maeneo Maalum ya mikusanyiko ya watu Wananchi waweze kupata huduma ya intanet bure.
Akizungumza na wananchi mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo ,alisema katika Jengo la Machinga Complex kuna Wafanyabiashara zaidi ya 4000 wanafanyabiashara zao katika jengo hilo wifi hiyo ya bure itawasaidia kutangaza biashara zao kwa kutumia wifi ya bure ya Serikali na kuelezea biashara wanazouza katika Jengo hilo la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
“Jengo la Machinga Complex wafanyabiashara na uongozi wa soko hili walikuwa wakitumia intanet ya kununua kuanzisasa intanet watatumia wifi ya bure pamoja na Wananchi wote ambao wanafika sokoni hapo kila siku kufuata bidhaa za jumla na rejareja katika soko hili la Serikali “alisema Mpogolo .
Mkuu wa Wilaya Mpogolo aliwataka Wananchi na wafanyabiashara watumie huduma za mtandao kwa Dhumuni sahihi ikiwemo kutafuta fursa za biashara na masoko ya ndani na nje .
Aliwataka Wafanyabiashara wa Machinga Complex kumpongeza Rais wa Dkt .Samia Suluhu Hassan na Waziri Nape Mnauye katika mikakati hiyo ya Serikali kuwasogezea huduma Wananchi za wifi.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary KUMBILAMOTO alisema Wafanyabiashara wa jengo la Machinga Complex kwa upendo wao wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, mwenye mapenzi na Watanzania wake
Meya KUMBILAMOTO alisema Wananchi wa Dar es Salaam wanapenda mseleleko hivyo wakifika katika jengo hilo kutumia intanet ya bure wasifukuzwe katika masaa yale ya kazi asubuhi mpaka jioni .
Meneja wa Soko la Machinga Complex Stella Mgumia, aliwataka Wafanyabiashara wamachinga kuondoka katika maene SI rasmi kwenda katika maeneo yaliotengwa na Serikali kuna fursa nyingi za biashara.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu