January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watendaji, wenyeviti watakiwa kutumia 4r

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online,Dar

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewataka Viongozi wa Serikali na Chama ngazi ya Matawi na Kata, kuwa na mahusiano mazuri kwa kusimamia 4r za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuwarahisishia utendaji kazi na kuwaletea maendeleo wananchi kwa haraka kwani pande zote hizo mbili zinategemeana.

Mpogolo ameyasema hayo leo Septembe 12, 2024 kwenye mkutano wa ndani alipokutana na Wenyeviti wa Mitaa na watendaji wa Mitaa, akiwataka kuimarisha uhusiano kati yao ili kuweza kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo, huku akibainisha kuwa kutokuwepo na uhusiano mzuri kati ya pande hizo mbili kunasababisha ucheleweshwaji waaendeleo.

“Ni vyema pande zote mbili kwa maana ya watendaji na wenyeviti mkawa na mahusiano mazuri ili muweze kutekeleza yale yote yaliyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025 ikiwemo ukamilishaji wa miradi ya maendeleo”, amesema Mpogolo.

Pia, amewataka watendaji kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa kwa viongozi wa Chama wa ngazi husika, huku akisema kuwa kufanya hivyo kunawarahisishia kuwafikia wananchi kwa urahisi ikiwa pamoja na kuyasemea yale yote yanayotekelezwa na Serikali.

Vilevile amewataka wananchi wa kata zote nne za Kitunda, Kivule, Kipunguni na mzinga na Wilaya ya Ilala kwa ujumla, kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya sita na kusema kuwa, Wilaya hiyo bado imeendelea kufanya vizuri katika sekta zote ikiwemo elimu, afya, miundombinu ya barabara, maji na umeme huku akisema kuwa, hadi sasa Wilaya hiyo imepokea zaidi ya Sh. Bil 304 kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya maendeleo.

Pia amesema kuwa, ndani ya kipindi kifupi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, imeweza kukusanya zaidi ya Bil. 111 fedha za mapato ya ndani, huku akisema kuwa fedha hizo zinaendelea kukamilisha miradi zaidi ya 280 iliyokatika Halmashauri hiyo.

Aidha,amewakumbusha kujiandikisha na kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la makazi linalotarajiwa kuanza Octoba 11 hadi 20, mwaka huu, huku a lani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuwaletea maendeleo wananchi ikiwa pamoja na kutatua kero zao