December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mpogolo awataka watendaji kuwa karibu na viongozi wa Chama

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online Ilala

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amewataka Watendaji wa Wilaya ya Ilala kuwa karibu na Viongozi wa chama na Serikali wasiwe sehemu ya vikwazo.

Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo, alisema hayo Tarafa ya Ilala wakati wa ziara yake ya kujitamburisha kwa Watendaji na Viongozi chama .

“Naomba Watendaji wa Tarafa ya Ilala mshirikiane na chama na Serikali katika kujenga mahusiano pamoja na wananchi msiwe sehemu ya vikwazo ndani ya Wilaya Ilala ” alisema Mpogolo .

Mkuu wa Wilaya Mpogolo alisema dhumuni la ziara hiyo kujitambulisha ,kujenga Mahusiano pamoja na kutatua kero mbalimbali zilizopo Wilayani humo .

Aliwataka Watendaji kushikamana na Serikali kutumikia wananchi katika utekekezaji wa Ilani katika kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kusimamia miradi ya Maendeleo ikiwemo ya sekta ya afya na sekta ya Elimu .

Aliwataka wakosoane kwa staha na kwa kupitia vikao vilivyowekwa badala ya kusemana katika vijiwe na mikutano ya Wananchi .

Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji, alimpongeza Mpogolo kwa mada nzuri Semina elekezi amewapatia Watendaji na Viongozi wa chama Ili kila mtu aweze jua Majukumu yake .

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ilala Habibu Nasser alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala watashirikiana naye katika utekekezaji wa Majukumu yake ya Chama na Serikali .