September 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mpogolo atoa Mikakati kuienzi Barabara ya Lumumba

Na Heri Shaaban, TimesMajira Onlie, Ilala

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, ametoa Mikakati kwa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuienzi Barabara ya Lumumba Wilayani Ilala .

Mkuu wa WIlaya Ilala Edward Mpogolo, alitoa agizo hilo kwa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Usafi wa Mwisho wa Mwezi Barabara ya Lumumba ambapo waliudhuria Watendaji wote wa halmashauri wakiwemo Watendaji madiwani Wakandarasi wa Kampuni za usafi Kajenjele na SATEK .

“Ninaagiza kwa Halmashauri ya Jiji tuweke utaratibu wa kuienzi Barabara ya Lumumba hii ni Barabara muhimu Barani Afrika ina historia Afrika ni jina la Kiongozi Patrick Lumumba “alisema Mpogolo .

Mkuu wa WIlaya Mpogolo alisema pia ukombozi wa Tanzania usingepatikana kwa ajili ya barabara hiyo toka wakati wa TANU baadae chama Cha Mapinduzi CCM .

Alisema kuanzia Leo Barabara ya Lumumba ni barabara Maalum kwa Viongozi wetu hivyo inatakiwa kuenziwa iwe Barabara ya kisasa.

Aidha alisema chama Tawala Cha Msumbiji FRELIMO harakati zao za Siasa walianzia Lumumba wakati huo walikuwa ndio wanafanya Siasa zao .

Alisema Mikakati yake ataongea na wadau kwa ajili ya kupanda Miti ya kisasa Ili kuipandisha hadhi Barabara ya Lumumba iweze kuvutia Eneo lote kuanzia Jumatano atafanya mkutano na Wafanyabiashara wa Lumumba Pamoja na Watendaji kwa ajili ya kuanza utekelezaji huo kuboresha Ilala iwe ya kisasa .

Alimwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam na Afisa Mazingira kuitisha kikao Arnatogluo kwa ajili ya mpango huo dhumuni kuungana na jitihada za Mkuu wa mkoa Dar es salaam za
kuipendezesha Jiji hilo katika utunzaji wa Mazingira .

Kaimu Mkurugenzi wa HALMASHAURI ya Jiji Amani Mafuru alisema kampeni ya usafi imefanya Tushike nafasi ya sita kwa usafi Barani Afrika .

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (Katikati )akiongoza Kampeni endelevu ya usafi Barabara ya Lumumba February 26/2023