January 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Ludigija awataka Watanzania kujenga umoja miaka 60 ya Muungano

Na Heri, Shaaban, TimesMajira Online

MKUU wa Wilaya ya Kwimba,Arch, Ng’wilabuzu Ludigija amewataka watanzania tujenge undugu na mshikamano na kudumisha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Ng’wabuzu Ludigija alisema hayo katika viwanja vya KWIDECO Kwimba wakati wa maadhimisho ya siku ya Muungano.

“Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania Bara ndugu zangu wana Kwimba tujenge undugu na mshikamano bila kujali kabila wananchi wote wa Kwimba tushikamane watu wasipandikize chuki “alisema Ludigija.

Mkuu wa Wilaya Ludigija alisema Hayati BABA wa TAIFA alisema wakati wa uhai wake Tanzania Bara na Tanzania Visiwani tusibaguane kizazi cheti dhambi hiyo aitaisha itatafuna vizazi vyetu hivyo aliwataka wawe wamoja na kujenga ushirikiano.

Aidha alisema Tanzania Bara na Tanzania Visiwani tunajivunia kuwa wamoja unaweza kugombea sehemu yoyote katika medani ya Siasa kwani huu ni Muungano wa Kiistoria bila kujali unatoka mkoa gani,Tanga au Kigoma lakini wote mnaishi Kwimba.

Alisema hata hapo Kwimba wapo Wanzanzibari wanafanya kazi sekta zote ikiwemo sekta Afya,Sekta Elimu, Usalama na wafanyabishara mbali mbali.

Alisema tunaendelea kumshukuru wasisi wa Taifa hili Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere, na Shekhe Abed Amani Karume unaweza kufanya kazi sehemu yoyote Tanzania Bara au Visiwani bila kubaguliwa na kudumisha umoja amani ya nchi yetu.