January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Kisare asisitiza TRA kuendelea kukusanya Kodi bila vitisho

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online


Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kisare Matiku Makori amesema kuwa anakumbuka kauli ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo amewataka maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi bila vitisho na hilo linajidhihirisha kwa kusema kuwa siku hizi TRA ni rafiki sana na wafanyabiashara na hilo ni jambo jema na lenye kudumisha uzalendo wa ulipaji kodi wa hiari.

Ameyasema hayo mwanzoni mwa wiki katika ofisi yake iyopo Moshi wakati alipotembelewa na maafisa kutoka TRA Makao makuu walipofika katika ofisi yake kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuanza ya zoezi la Elimu ya kodi Malngo kwa Mlango kwa wafanyabiashara wa Moshi sambamba na kusikiliza changamoto zao ili waweze kuzifanyia kazi.

Mh. Kisare Matiku amesema kuwa anafurahia kuwepo kwa elimu ambayo itawafikia wafanyabiashara moja kwa moja katika maeneo yao ya biashara na kuwataka wafanyabiashara hao kushirikiana na maafisa wa TRA ili kufikia lengo lilokusudiwa.

“Natoa pongezi kwa hatua waliyofikia Maafisa wa TRA ya kukusanya kodi bila Mitulinga kama maagizo ya Mh. Rais yalivosema kwaajili ya faida ya Nchi yetu na maendeleo ya Taifa letu, pia kama tujuavyo Serikali haina biashara yoyote isipokua kodi, hivyo utoaji wa elimu ni hatua kubwa sana na itaongeza “sovereignty” na uwezo wakulipakodi utaongezeka.”

Nae kiongozi wa zoezi hilo, Afisa Mkuu Elimu kwa Walipakodi na Mawasiliano Bi. Lydia Shio kutoka TRA Makao Makuu amesema uwepo wa maafisa ni kutoa elimu ya kodi na kusikiliza changamoto zao ambazo hata wao wanashindwa kuzileta katika ofisi zao hivyo wameamua kuwafata katika maeneo yao ili kujua uhalisia wa biashara zao na kuwakumbusha malipo ya kodi kwa hiari.

“Tumekuja kwa lengo la kutoa elimu kwa Walipakodi na wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro tukianzia na Wilaya ya Moshi Mjini ili kuwakumbusha walipakodi waweze kujua wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati kwaajili ya kuongeza pato la Taifa, wafanyabiashara wengi wamesema kua huko nyuma walikua wakiwaona maafisa kutoka TRA wanawakimbia na hawajui wanakimbia kwa kosa gani ila kwa sasa hawana haja ya kukimbia maana tukifika wanatusikiliza na kufanya kilichotuleta na wao wanauliza maswali na kuwasilisha changamoto zao kwa ufafanuzi Zaidi ili aweze kulipakodi inavotakiwa”

Mmoja wa wafanyabiashara wa mtumba katika eneo la soko kuu la Memorial Bi. Betty Urono ameeleza kuwa yeye anatumia machine ya risiti na inamsaidia sana na angependa kuwaona wafanyabiashara wenzake wanatumia pia ili kulipakodi kwa usahihi na kujenga taifa letu na maendeleo ya nchi.

“mimi natumia machine ya risiti EFD ni nzuri na inasaidia sana katika kutunza kumbukumbu zetu ni nzuri katika bishara yangu, mimi natoa risiti na nawaomba wengine pia watoe risiti kwa faida yao na ya Nchi yetu pia.”

Mkoa wa Kilimanjaro umekua ni moja wapo ya mkoa wenye historia nzuri katika ulipaji na ukusanyaji kodi na kufikia malengo na muendelezo wa gurudumu la kuongeza pato la Taifa na maendeleo kiujumla hii ni kutokana na ushirikiano unaopatikana kutoka kwa wafanyabiashara na taasisi ya TRA ya Mkoa wa Kilimanjaro katika kutimiza malengo ya Serikali yetu katika kuendeleza maendeleo ya Mkoa na Nchi kiujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mh. Kisare Makori Akiongea na Timu ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu waliofika katika ofisi zake kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuanza kwa kwa zoezi la kutoa Elimu ya Kodi ya Mlango kwa mlango kwa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro