September 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Kheri James: Wafanyabiashara changamkieni fulsa ya mikopo itolewayo na Halmashauri

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Mbulu

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara Komred Kheri James amewataka wafanyabiasha mbalimbali wa Soko la Mbulu Mjini kuhakikisha wanachangamkia fulsa ya mikopo itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.

Hayo ameyazungumza Jana wakati alipokua akizungumza na wafanyabiasha mbalimbali wa Soko kuu la Mbulu Mjini, ambapo alisema kufanya hivyo kutasaidia kuongeza miraji lakini pia kukuza Uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Komred James amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suhulu Hassan inatoa mikopo kwa Wanawake, Vijana, na Watu wenye ulemavu, hivyo ni vema wafanyabiasha wakachangamkia hiyo fulsa ili kuweza kukuza miraji ya Biashara zao.

Aidha alisema Biashara yoyote ile inahitaji mitaji na nidhamu ya matumizi ya fedha katika kuiendesha Biashara husika, hivyo wafanyabiasha wahakikishe wanakwenda Halmashauri kuchukua mikopo ili waweze kukuza na kuendekeza Biashara zao kikamilifu.

Mbali na hilo pia amewataka wafanyabiasha hao kuhakikisha wanazingatia suala la Usafiwa Mazingira ya soko, ikiwa ni sambamba na kuwa wabunifu wa Biashara wanazoziendesha.

Komred Kheri James amefanya ziara katika Eneo la Soko Kuu la Mji wa Mbulu ambapo amepata fulsa ya Kutembelea Mazingira ya Soko hilo na Kuzungumza na Wafanyabiashara Sokoni hapo.

Aidha pamoja na mambo mengine amesikiliza Kero, Ushauri na Maoni ya wafanya biashara yaliolenga kuimarisha uendeshaji wa Soko na Usimamizi wa biashara katika Soko hilo.

Komred James uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu kuendeleza Utamaduni wa kusikiliza na kufanyia kazi Kero na maoni mbalimbali ya wafanyabiashara pamoja na Kuweka Mpango wa mkakati wa Ukarabati, Usimamizi na Maboresho ya Mazingira ya Biashara Katika Soko hilo.

Mbali na hayo pia Mkuu wa wilaya huyo akiwa Ofisini kwake amefanya Mazungumzo na Wabunge wa Majimbo Mawili ya Wilaya ya Mbulu Kujadili Masuala mbalimbali ya ya Maendeleo ya majimbo yote mawili ya Mbulu.

Komred Kheri amewapongeza Wabunge hao kwa Kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ya Kupigania Maendeleo ya Wananchi wa Wilaya ya Mbulu na amewahakikishia kuendelea kutoa ushirikiano mbalimbali katika kusimamia na kuongeza kasi ya Maendeleo na kuwatumikia Wananchi hao kikamilifu.