December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Ilala kuzindua kupima Afya bure Ilala

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija anatarajia kuzindua kampeni ya kupima Afya Bure wananchi wa Wilaya ya Ilala Dar Salaam .

Kampeni hiyo ya kupima Afya Bure inatarajia kuzinduliwa Juni 11 mpaka 12 mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Wilayani Ilala.

Akizungumza kampeni hiyo ya kupima Afya Bure Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dkt.Eldhabeth Nyema alisema Kampeni hiyo Halmashauri ya Jiji wameshirikiana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa Dar es Salaam kwa dhumuni la kupatatia matibabu Bure ya magonjwa mbalimbali.

“Kampeni hii ya kupima Afya Bure itafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja zoezi litakuwa siku mbili kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa ambapo madaktari Bingwa wa magonjwa mbalimbali watakuwepo siku hiyo hivyo Wananchi mnaombwa kujitokeza kwa wingi”alisema Dkt.Eldhabeth .

Dkt Eldhabeth alisema tayari wameshajipanga na madaktari Bingwa kwa ajili ya zoezi hilo la kupima Afya Bure amewataka Wananchi kujenga tabia ya kuangalia Afya zao Kila wakati.

Dkt Eldhabeth alisema Afya yako mtaji wako hivyo kuangalia Afya Kila wakati ni muhimu kwa ajili ya kuangalia magonjwa mbalimbali yaweze kupatiwa matibabu na madaktari wetu.