Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija ameagiza WATENDAJI wa Halmashauri ya Jiji wote kutoa ushirikiano na Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala katika Utekelezaji wa majukumu yao ya kazi
Mkuu wa Wilaya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija alitoa tamko hilo katika Kampeni ya Jumuiya ya Wazazi ya upandaji miti 5000 katika uzinduzi uliofanyika Shule ya Sekondari ya Jumuiya ya Wazazi Tabata Kimanga Wilaya ya Ilala.
“Kukua kwa CCM kwa ajili ya Jumuiya, Jumuiya ya Wazazi ina jukumu kubwa sana naagiza kwa Watendaji wa Kata na Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa kazi zinazofanywa na Jumuiya ya Wazazi kwani Jumuiya ya Wazazi ni Mzizi wa Malezi ya Familia” alisema Ludigija.
Lugigija alisema malezi ya familia yananzia ngazi ya Kata na mitaa hivyo Jumuiya hiyo ina jukumu kubwa sana kushirikiana na Watendaji wa Serikali katika kufatilia Maendeleo ya watoto ikiwemo shule.
Aliwapongeza Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe na Katibu wake wameupiga mwingi katika uwandaji wa kampeni ya kupanda miti 5000 kuipendezesha Wilaya llala ya kijani .
Alipongeza Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala na Kamati ya Utekelezaji kwa kumuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Samia Suluhu Hassan katika utunzaji wa Mazingira.
Aliwagiza viongozi waliopewa dhamana kusimamia utunzaji wa miti hiyo Kwa ajili ya kuipendezesha Jiji letu .
Alisema mabadiliko ya tabia ya nchi yana athiri nchi yetu kwa kiasi kikubwa kutokana na uharibifu wa Mazingira mkaa ni zao la misitu na Dar es Salaam ni watumiaji wakubwa wa rasilimali ya misitu .
Aliwataka wananchi wa Wilaya ya Ilala kila kaya kupanda miti mitano ikiwemo ya matunda na kivuli
Akizungumzia kampeni ya wilaya ya ilala kila mwaka wanapanda miti milioni 1.5 .miti mbalimbali ya matunda ikiwemo ya kuzuia momonyoko na miti ya vivuli
Mwenyekiti wa JUMUIYA ya wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe alisema miti hiyo 5000
KAMPENI ya Ilala ya kijani itasambazwa kila kata miti 20 ,ngazi ya matawi miti 15, Wilaya ya Ilala ina matawi 265 ya Jumuiya ya wazazi.
Aliwataka viongozi wake wa Jumuiya kupanda miti hiyo Shuleni,katika vituo vya Afya na Ofisi za SERIKALI, Kamati ya Utekelezaji wilaya itakuwa inafanya ziara kufatilia Maendeleo yake mpaka inakuwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Tabata Kimanga Zayana Rashid alipongeza Viongozi wa Wilaya wa Jumuiya na serikali katika kufanikisha kampeni ya Ilala ya Kijani.
Zayana amewataka viongozi wa Jumuiya hiyo kusonga mbele katika kutekezaji wa majukumu yao ikiwemo upandaji miti Kwa ajili ya utunzaji Mazingira na kuimalisha Jumuiya vizuri
More Stories
Wanaoficha watoto wenye ulemavu kusakwa
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali