Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amepiga marufuku Mgambo wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kukamata wamachinga na kuondoka na bidhaa zao badala yake amewataka Mgambo wa Halmashauri hiyo wawaelekeze wamachinga sehemu sahihi za kufanya biashara ambazo zimetengwa na Serikali.
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo alisema hayo wakati wa siku ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan iliyoandaliwa na Uongozi wa soko la Machinga Complex wilayani Ilala leo.
“Nawaomba Mgambo wa Halmashauri ya jiji marufuku kukamata bidhaa za wamachinga mama Lishe mkaondoka nazo badala yake nawaomba mnapowakamata muwape elimu na kuwaelekeza sehemu rasmi za kufanya biashara “alisema MPOGOLO
Mpogolo alisema mgambo wa Halmashauri uwezi kukamata bidhaa za wamachinga na kuondoka
nazo sababu ujui pesa ya mkopo wamepata wapi badala yake jukumu la kubwa la Mgambo kutoa elimu .
Aliwataka wafanyabishara Wilaya ya Ilala kupendana na kujenga mshikamano pamoja na kupenda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwaunganisha na taasisi za kibenki na kuwawezesha kupata mikopo ya Benki na Serikali kupitia Halmashauri.
Alisema sasa hivi Wamachinga wanakopesheka Rais amekuza uchumi katika nchi yetu na kujenga Demokrasia na amedumisha umoja na mshikamano na kuleta fursa za uchumi.
Mkurugenzi wa soko la Machinga Complex Stella Mgumia alisema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anawapenda wafanyabishara wamachinga ndio maana amewaunganisha pamoja ili waweze kutambulika na kupata fursa za kiuchumi.
Aidha Mkurugenzi Stella alimpongeza mama Mzazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia ametuletea Rais mchapakazi mwanamke mwezetu ambaye anafanya kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani na kujenga nchi .
More Stories
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta