December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Daraja la Tabata kisiwani kujengwa April 2024

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,amesema daraja la barabara ya Tabata Kisiwani linalounganisha wilaya ya Ubungo linatarajia kujengwa Aprili 2024 kwa ajili ya kuunganisha mawasiliano ya eneo hilo kuwaondoa wananchi katika adha wakati wa Mafuriko.

Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli ,alisema hayo katika ziara yake jimbo la Segerea wakati wa kugagua miundombinu ya Barabara ya TABATA, Bonyokwa, Kinyerezi, ambazo zimeathilika na mvua .

“Daraja la Mwananchi Tabata Kisiwani litajengwa April 2024 na mradi wa kisasa wa kuboresha miundombinu ya jiji ambao unafadhiliwa na benki ya Dunia tunajenga daraja hili lipo katika mpaka wetu jimbo la segerea linaunganisha wananchi wangu wa Kimanga na Tabata “alisema Bonah.

Mbunge Bonnah alisema katika wilaya tano mradi wa kuboresha miundombinu ulikuwa aupo ulikataliwa na madiwani 2015 madiwani walikataa mradi ulienda Temeke ndio maana barabara zetu zimekuwa mbovu mwaka 2020 mradi umesainiwa lakini umechelewa barabara hiyo ya Kisiwani Tabata mwananchi daraja litajengwa na TARURA ina pesa nyingi mradi kweli ulichelewa ulitakiwa kuanza September lakini taratibu za Serikali ndio ukachelewa kuanza kwa wakati .

Mbunge Bonnah alisema Serikali imeshatoa pesa ya mradi wa kisasa hivyo hawawezi kutoa pesa tena kwa ajili ya mitalo daraja lipo ubungo linajengwa na Ilala lina wananchi wengi jimbo la Segerea litakapoisha litafungwa taa za kisasa .

Akizungumzia kata ya Bonyokwa alisema Bonyokwa ni Kata ambayo aina lami ,Makoka na eneo la Masisita pesa za zarula zitaelekezwa kujenga pia ameomba pesa ya zarula kujenga kipande cha zahanati kiwango cha lami baadae wamwage zege.

Alisema dhumuni la ziara hiyo kuangalia athari za mvua zilivyoharibu miundombinu ambapo barabara ya Bonyokwa ipo katika mikakati ya kujengwa.

Meneja wa TARURA wilaya ya Ilala Silvester Chinengo alisema TARURA Wilaya ya Ilala wamepokea maelekezo ya Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli kwa ajili ya kuomba pesa za zarula kwa ajili ya Barabara bajeti ijayo barabara zitajengwa kwa kiwango cha zege.

Meneja Chinengo alisema ujenzi wa barabara ya Kipande cha Bonyokwa umesimama kwa ajili ya mvua mvua ,mvua zitakapomalizika ujenzi huo utamalizika amewataka wananchi kuwa watulivu Wauunge mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.