Na Mwandishi wetu,Timesmajira
KATIKA kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, Mkoa wa Dar es salaam unatarajia kufanya kongamano maalum machi nne mwaka huu katika ukumbi wa Ubungo Plaza lengo likiwa ni kuikumbusha jamii kutambua na kuthamini nafasi ya mwanamke sanjari na kuhamasisha usawa
Akizungumza leo Machi 3,2025 Jijini Dar es salaam na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema maadhimisho ya mwaka huu yanakwenda sanjari miaka 30 ya utekelezaji wa ulingo wa Beijinn katika kuhamasisha usawa hivyo amewataka wanawake kujitokeza kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhamasisha usawa
Chalamila amesema kuwa wakati maadhimisho ya kitaifa yakiwa yanatarajia kufanyika machi nane Mkoani Arusha, ambapo Mkoani Dar es salaam maadhimisho hayo yatafanyika kwenye viwanja vya Leaders Club na zaidi ya mitungi elfu moja ya Gesi itagawanywa bure kwa wanawake ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi za Rais Dokta Samia kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia na kulinda afya za wanawake.

Aidha Chalamila amesema kuwa serikali inatambua nafasi ya mwanamke na imetenga maeneo maalum kwa wanawake kufanya biashara za vyakula kipindi cha mfungo hivyo amewataka wanawake kutumia fursa hiyo pamoja na fursa zingine zilizopo kwenye biashara saa 24.

Hata hivyo Chalamila amewataka wanawake kutumia fursa za mikopo ya Halmashauri kupitia Benki mbalimbali na kusisitiza kuwa katika kutambua nafasi ya mwanamke serikali nchini Tanzania imewatengea wanawake mikopo maalum ambayo ni asilimia nne kutoka kwenye Halmashauri zote nchini
Maadhimosho ya kitaifa ya siku ya wanawake hapa nchini yanatarajia kufanyika machi nane mwaka huu Mkoani Arusha ambapo Rais Dkt Samia anatarajia kuwa mgeni rasmi.
More Stories
Mpina,Maganga kuendelea kuwafichua viongozi mafisadi na wabadhilifu
Wakazi Mahomanyika wamlilia Rais Samia kuingilia kati mgogoro wa ardhi
Sheria kuitambua maabara Tume ya Madini