Na Zena Mohamed, TimesMajira Online, Dodoma
KUFUATIA kukua kwa teknojia ya Mawasiliano nchini,hivi sasa Benki ya CRDB imefanya maboresho ya huduma zake ambapo mwananchi yeyote anaweza kufungua akaunti ya benki hiyo kwa kutumia simu ya kiganjani popote alipo na kuepusha usumbufu.
Hayo yameelezwa jijini Dodoma leo na Meneja Mafunzo na Maendeleo ya benki hiyo, Edith Mwiyombela wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya pili ya elimu na Ufundi yaliyoandaliwa na Baraza la elimu Tanzania(NACTE) yanayoendelea katika Viwanja vya Jamhuri.
Akiongea katika maonyesho hayo amesema, wamefanya maboresho katika huduma za kifedha na kuwa rahisi ikiwa ni pamoja na kupunguza masharti kwa wateja.
Amesema,huduma hiyo itaondoa vikwazo ambavyo wateja wengi huona kama kero kwao ikiwepo barua ya wadhamini ,barua ya Mtendaji,picha ya paspoti pamoja fedha ya papo kwa papo ambapo kwa sasa unaweza kufungua akaunti kisha ukahamisha fedha kutoka kwenye mitandao ya simu kwenda kwenye akaunti.
“Huduma hii imerahisisha sana,kwanza mteja atakuwa ameokoa muda,wateja wengine walikuwa wanatamani sana kufungua akaunti, lakini walikosa muda,wakati mwingine walitumia muda mwingi katika kutimiza vigezo au kukosa kabisa,”amesema.
Kwa upande wake, Simon Mukajanga ambaye ni mshirika wa programu ya uzamili katika benki hiyo ameeleza vigezo na masharti vya kufanikisha kujiunga na huduma hiyo ya kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi bila kufika Ofisi za Benki ambapo amesema mteja atatakiwa kutumia namba ya kitambulisho cha uraia (NIDA) ili kujifungulia akaunti mwenyewe.
Pamoja na hayo alifafanua kuwa, huduma hiyo ina faida kwa kuwa inatoa risiti kwa njia ya simu ili kumrahisishia mteja kuwa na kumbukumbu ya miamala aliyoifanya na kuifanyia mipango katika maendeleo yake.
“Risiti inasaidia mtu kupangilia mipango yake katika matumizi,tunawashauri wananchi kuitumia huduma hii kwani inaokoa muda kwa kuwa huhitaji kusafiri ,utatumia simu yake huku akiendelea na mambo mengine ya uzalishaji,”amesistiza.
More Stories
Asilimia 64.35,ya wafanyabiashara wabainika kutokuwa na leseni
UAUT wajipanga kuzalisha wanafunzi waliopikwa vizuri
Wanafunzi 7176, kufanya mtihani wa taifa