Na Penina Malundo,timesmajira,Online
BODI ya Nafaka Tanzania (CPB) imesema dhamira yake ni kuhakikisha mkulima mdogo anapata bei shindani katika mazao yake na inauwezo mkubwa wa kuweza kununua mazao ya mkulima kwa bei shindani kwa kufanya uchambuzi na kujua mkulima anatumia gharama gani shambani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, Mkurugenzi Mkuu,Dkt. Anselm Moshi amesema bodi yao imekuwa ikihakikisha mkulima anakuwa na masoko ya uhakika na kujenga viwanda kwa wingi.
Amesema wamekuwa wakijenga viwanda kila mahali na kuongeza kasi hiyo ili viwe soko ya mkulima katika kuuza mazao kwa urahisi.
Amesema ujenzi huo wa viwanda utaweza kutoa fursa kwa vijana kupata ajira na thaman ya mazao yao wanayozalisha yanaweza kuuzwa katika masoko ya kimataifa na kuleta fedha katika nchi.
“Tukileta fedha nyingi katika nchi tutahakikisha mfumo wa bei unakuwa imara hauyumbiyumbi sana,”amesema na kuongeza
Amesema wakulima wengi kwa sasa wanamikataba mingi katika maeneo yao ambapo wapo 60,000 katika kilimo cha ngano ,alizeti ,maharage ya soya.
Aidha amesema tangu mwaka juzi wameanza mikakati ya kilimo cha mikataba kuhakikisha kwamba wanafanya uhamasishaji wakulima waweze kulima na wizara ya kilimo kuhakikisha wakulima wanapata mbolea na pembejeo za wakati.
Amesema katika nchi kilimo cha ngano kilianguka na kukawa hawazalishi hivyo wakawa wanategemea kwa kiasi kikubwa kuagiza kutoka nje .”Tunaagiza sasa hivi ngano tan milioni 1 kila mwaka ambazo tunatumia fedha za kitanzania Bilioni 530 kila mwaka …tunamaelekezo ya serikali ya kuhakikisha wanazalisha ngano ya kutosha Tanzania tufikie angalau tani Miliono 1 na zaidi ifikapo mwaka 2025.
 “Tumeanza mwaka jana tumeanzisha mbegu kutoka Zambia tani 204 na kugawa kwa mkopo ile kanda ya kasikazini na matokeo yalikuwa mazuri,”amesemaÂ
More Stories
Simbachawene:Waombaji wa ajira jiungeni na Mfumo wa Ajira Portal
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki