Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Arusha
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesema Ngorongoro ni ngome ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hakuna chama mbadala kitakacho watatulia kero wananchi wa eneo hilo.
CPA Makalla, ameyasema hayo leo, Septemba 6, 2024 kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Mazingira Bora, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 6 katika Wilaya ya Karatu, Longido, Monduli.
Amesema, baada ya mrejesho aliopata baada ya kikao cha ndani alichofanya na baraza la madiwani na wajumbe wa Kamati ya siasa Ngorongoro, ambapo wajumbe hao wameeleza kuonesha kuridhishwa na mwenendo wa CCM huku wakidai kuendelea kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pia CPA Makalla amesema, kutokana na Maendeleo yanayofanywa na Serikali ya CCM wananchi wa Ngorongoro kupitia viongozi hao, wameahidi kuendelea kukiunga mkono chama cha CCM na kusema kuwa hakuna chama mbadala kitakachoweza kuwaletea maendeleo.
Aidha, CPA Makalla amesema kuwa, mbali na kutoweza kufika Wilaya ya Ngorongoro kutokana na zuio la Jeshi la Polisi lililotolewa hivi karibuni, amesema bado CCM inatambua mchango wa wakazi wa eneo hilo na kuahidi kuendelea kupeleka maendeleo na chama hicho kitajitahidi kufika pindi watakaporuhusiwa.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best