Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makala amesema amemsikia Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe Akieleza kuwa Chama chake hakina Ilani hivyo kuwataka wagombea wa Chama hicho kubuni Ilani pindi watakapo chaguliwa.
CPA Makala ameyasema hayo leo Novemba 20,2024 mbele ya wananchi wakiwemo wana CCM wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akizindua kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajia utafanyika Novemba 27 mwaka huu.
Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi hao CPA Makala amesema, amefuatilia hotuba ya Mbowe jana na amemsikia akisema Chama chake hakina Ilani na ameagiza kila mgombea atakayeteuliwa katika Kijiji chake au katika mtaa wake abuni Ilani yake
“jana nilikuwa namfuatilia Mbowe kwenye hotuba yake na chakushangaza zaidi amesikika akisema chama chake cha CHADEMA hakina Ilani na hakiwezi kuandika, hivyo amewataka wagombea wake endapo watashinda katika uchaguzi kwenda kubuni buni Ilani ya Mtaa na kwenye Kijiji pia huyo kiongozi wao abuni Ilani ya sehemu hiyo.
“Kwahiyo mnaweza kupata picha mnaenda katika uchaguzi kuna Chama kimeleta maendeleo na mafanikio, kuna chama kina Ilani lakini kuna chama kingine kinakuja kuomba kura lakini kinawathibitishia watanzania kwamba wao hawakujipanga na wanataka wagombea wao wabuni Ilani katika kijiji anachokaa, mnakuwaje na kiongozi anaye lala na kuamka anabuni Ilani? Alimaliza kwa kuuliza.
“Pamoja na Ilani sisi Chama Cha Mapinduzi tumetoa tamko la kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hawa wagombea wetu watakuwa wanajinadi lakini watakuwa wanatumia tamko la Chama Cha Mapinduzi.”
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam