NA Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA, Amos Makalla, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuhakikisha Sekta ya usafirishaji inazidi kukuwa kila siku.
CPA Makalla, ameyasema hayo leo Julai 13, 2024 aliposafiri kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa Treni mpya ya mwendokasi (SGR) na kusema usafiri huo ni mzuri na unamrahisishia msafiri kufanya shughuli zake kwa urahisi kati ya Mkoa mmoja hadi mwingine kwa kufika kwa wakati.
Amesema, amefurahi kuwa miongoni mwa abiria waliosafiri na treni ya SGR kutoka Morogoro mpaka Dar es salaam na kuongeza kuwa ni Treni nzuri yenye huduma nzuri na haichoshi.
“Nakumbuka nilikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakati Mhe Samia suluhu Hassan anachukua Urais, kipande hiki cha Dar es salaam Morogoro kwa wakati ule kilikuwa asilimia 42 lakini amefanya kazi kubwa na kwa sasa kimekamilika na wakati wote naambiwa itazinduliwa safari za Dar es salaam mpaka Dodoma”amesema Makalla
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato