COSTECH yafadhili mradi utafiti matokeo mabaya somo la hisabati kidato cha nne na darasa la saba
Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH)
TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imesema kuonekana na kuwepo kwa changamoto ya matokeo mabaya ya somo la hisabati katika matokeo ya Darasa la Saba na kidato Cha nne tume hiyo imefadhili Mradi wa utafiti ili kugundua sababu ya tatizo hilo.
Hayo yameelezwa jijini hapa leo ,Agosti 25,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Dkt.Amos Nungu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli na mafanikio ya tume hiyo.
“Somo la hisabati bado linaonekana ni changamoto kwani matokeo yake yamekuwa mabaya Kwa kidato cha nne na Darasa la nne hivyo kwa kubaini chanzo cha tatizo hilo sisi kama Tume tumeidhinisha miradi miwili ambayo kila mmoja thamani yake ni milioni 120,”amesema Dkt.Nungu
Vilevile Dkt.Nungu ametaja baadhi ya shughuli zilizotekelezwa na Tume hiyo kuwa ni pamoja na kuibua na kufadhili miradi ya kimkakati ambayo tayari michakato yake imefanyika na sasa ipo katika hatua ya mikataba ambapo Serikali kupitia COSTECH imeidhinisha jumla ya miradi saba kwa thamani ya shilingi milioni 150 kila mradi.
Amesema Miradi hiyo itafanyika ndani ya miaka miwili na inahusisha watafiti na wabunifu kutoka sekta zote za umma na binafsi.
Aidha amesema kuwa Serikali kupitia COSTECH, imeidhinisha miradi miwili kwa thamani ya shilingi milioni 120 kila mradi ambapo utekelezaji wake pia unahusisha watafiti kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini na itafanyika ndani ya miaka miwili, sasa ipo hatua ya kusaini mikataba.
“Serikali ilifadhili miradi ya utafiti kupitia COSTECH, baadhi ya miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na Tume inafanya ufuatiliaji wa miradi inayohusu kuboresha maabara za utafiti kwa ukarabati na ununuzi wa vifaa vya kisasa ikiwemo, Maabara ya Utafiti wa Baharini katika Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar mradi ambao tayari ulishakamilika,”amesema Dkt.Nungu
Akizungumzia majukumu na vipaumbele vya tume hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, Dkt.Nungu amesema kuwa Tume hiyo imeendelea kusimamia miradi inayoendelea ukiwemo wa Kigoda cha Utafiti katika SUA na NM-AIST ambao ni mradi wa miaka mitano, wenye thamani ya takribani shilingi bilioni 5 pamoja na kushirikiana na Mabaraza ya Kikanda na Kimataifa kuhakikisha tunashiriki kutafuta fursa ambazo zitaendelea kuleta fedha za utafiti kupitia COSTECH au kuhamasisha Taasisi za ndani kuomba hizo fursa.
Kukamilisha zoezi la ufadhili wa pamoja miradi ya utafiti wa Mabaraza ya Utafiti duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuongeza kuonekana kwa watafiti wetu na kuitangaza nchi yetu katika nyanja hii ya utafiti pamoja na kukamilisha mchakato na kutoa fedha kwa maandiko mawili kwa kutoa mrejesho kwa walioshiriki lakini wakakosa, na kuwatembelea walioshinda.
Vilevile, kupitia mradi wa HEET, tunaboresha mifumo mbalimbali ili kuongeza ufanisi zaidi katika suala la uratibu wa ume. Ikumbukwe kuwa mradi huu ni mahususi kwa Taasisi za Elimu ya Juu hivyo, inabidi tuwe tayari kuwahudumia baada ya kukamilisha mabadiliko wanayofanya kupitia mradi huo.
More Stories
Wasira :Uamuzi Mkutano Mkuu umezingatia katiba
Wajumbe Mkutano Mkuu Maalum wapongezwa
Wavuvi 540 waokolewa Ziwa Rukwa