January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CLUB ya Waandishi Wa Habari Rukwa yafanya mabadiliko madogo ya katiba yao

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Rukwa

CLUB ya Waandishi Wa Habari Mkoani Rukwa imefanya mabadiliko madogo katika katiba Yao kwa kuongeza baadhi vipengele ambavyo havikuwemo katika katiba Yao ilikuendana na mazingira ya sasa kiutendaji.

Mkutano mkuu WA dharura uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita uliweza kukubaliana kufanya marekebisho katika vipengele vitatu ambapo kamati ya nidhamu,maadili na usuluhishi lmebaki kuwa kamati ya nidhamu na maadili na kuongeza kipengele Cha kamati ya utatuzi WA migogoro.

Pia katika mkutano mkuu huo waliweza kupitisha azimio la uanzishwaji WA Kikoba ambacho kitaanza mapema January,2024 katika kukabiliana na changamoto za umasikini katika tasnia hiyo ya Habari.

Akitoa ufafanuzi katika mkutano mkuu huo mwenyekiti WA Club ya Waandishi WA HABARI mkoa Rukwa Nswima Ernest alidai kuwa marekebisho hayo ya katiba yametokana na mkutano mkuu WA UTPC ambao ulipendekeza Vilabu vya Waandishi WA HABARI kufanya mabadiliko hayo ya katiba Ili kuendana na mabadiliko ya kiutendaji katika Vilabu vyote vya Waandishi WA HABARI Nchini.

Alidai kuwa mabadiliko hayo ya katiba ni sehemu ya mabadiliko ya kimfumo katika uendeshaji WA Vilabu vya Waandishi wa Habari Ili waweze kuwa na nafasi ya utatuzi wa migogoro ndani ya Vilabu vyao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa Waandishi WA Habari wanaimarishwa katika eneo la uchumi Kwa kuwa taasisi ya fedha yenye nguvu itakayowawezesha kulipa na kuendesha shughuli zao za kiuchumi.

Katika mkutano mkuu huo wajumbe waliweza kufanya uchaguzi WA kuwapata Wajumbe watano wa kamati ya usuluhishi na utatuzi wa migogoro ambao ni Fatuma Mkumbo,Latius Bazigazi,Jellad Sylivesta,Juliana Timotheo na Peter Malema.

Na kamati ya Nidhamu na Maadili ni Franco Nkyandwale,Jane Mwakyoma,Israel Mwaisaka na Gulian Adolph.

Mabadiliko hayo ya katiba ambayo yamebarikiwa na mkutano mkuu ni mkakati WA pamoja WA Vilabu vyote vya Waandishi wa Habari HAPA Nchini katika kupiga hatua mbele zaidi na kujenga taaluma ya Waandishi WA Habari yenye nguvu na weredi mkubwa.