January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kuja na elimu ya upigaji dawa

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

MHANDISI mitambo na viwanda wa Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) Mhandisi, Yeremia Gwau amesema kuwa Chuo hicho kimekuja na teknolojia za kisasa za kuboresha sekta ya kilimo kwa kutoa elimu ya upigaji wa dawa kwa kutumia vifaa vya kisasa kwa wakulima mashambani.

Mhandisi Gwau amesema hayo leo wakati akizungumza na hili kwenye banda la Maonyesho ya sikukuu ya wakulima nane nane ambayo kitaifa inafanyika Jijini Mbeya.

Hata hivyo Mhandisi Gwau amesema kuwa kwa kuzingati changamoto za kitafiti katika uzalishaji Chuo hicho kina programu maalum ya kuangalia changamoto katika sekta ya kilimo na kuzitafutia majawabu lengo ni kuhakikisha inakuwa na wakulima kunufaika.

Eliwanzita Sospeter ni Mtaalam wa Teknolojia ya Chakula (MUST ) amesema kuwa wanatumia teknolojia za kisasa bunifu ya uzalishaji wa majokofu ambayo mkulima au mfanyashara ana uwezo wa kutunza mbogamboga na matunda kwa zaidi ya wiki moja pasipo kuharibika au kuathirika na wadudu.

Amesema kuwa ni Teknolojia ambayo ni rahisi kwa mkulima yeyote anasema kutumia na kuwa katika msimu wa maonyesho ya wakulima wamedhamiria kufanya ubunifu ili kuweza kuwasaidia wakulima.

Eliwanzita amesema kuwa katika msimu wa maonyesho haya Chuo cha Must wamejidhatiti kufanya ubunifu wa aina mbalimbali wenye kuleta matokeo mazuri katika Sekta ya kilimo.

Michael Raphael ni mkulima wa mboga mboga katika kata ya Igurusi amesema kuwa uwepo wa wataalamu kutoka Chuo cha Must umekuja Muda muafaka kwako kwani utaweza kuwasaidia katika uzalishaji pamoja na kilimo cha kisasa.

“Unajua ndugu mwandishi wakulima tuliowengi huko Vijijini tunajilimia tu bila kufuata taratibu za watalaam uwepo wa maonyesho haya naamini utatusaidia wakulima tulio wengi kubadilika baada ya kupata elimu”amesema.