Na Mwandishi wetu, timesmajira
KATIBU Mkuu Wizara ya Maji Prof.Jamal Katundu amekitaka Chuo cha Maji kuhakikisha wanazalisha vijana wenye uwezo mzuri ambao wataweza kutatua changamoto zinazokaikabili sekta ya maji nchini.
Pia ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha Walimu wanaowafundisha wanafunzi hao kuwawekea kigezo cha wao kufanya tafiti na machapisho mbalimbali ambayo yataweza kwendana na wakati katika kufundisha wanafunzi hao.
Ameyasema hayo jana,Novemba 2,2023 jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 46 ya Chuo cha Maji,Prof, Katundu alisema ongezeko la udahili la wanafunzi hao katika chuo hicho linapaswa kwendana na ubora wa elimu.
Amesema mbali na utoaji wa elimu pia walimu wanaowafundisha wanafunzi hao wanapaswa kufanya tafiti mbalimbali,kutoa ushauri pamoja na kuwa na machapisho ambayo yataweza kusaidia kuonesha walimu hao ni wabobezi wazuri katika sekta hiyo.
”Imani ya serikali kuona chuo kitajikita na tafiti kuleta suluhisho,tafiti hizi hata kwa walimu zitakuwa sababu yao kupandishwa vyeo vyao,niombe wanataaluma na mkuu wa Chuo kuhakikisha mnaweka vigezo kwa walimu hawa,kwani itakuwa ni vitu vya ajabu kama tunamwalimu anamiaka sita hajawahi kufanya utafiti,ushauri alafu anafundisha wanafunzi,”amesema
Amesema wanapaswa kuweka utaratibu ambao utawahusisha walimu wote na endapo hajiusishi kwenye utafiti wala kwenye machapisho akaendelea kufundisha watoto kwa sababu atakuwa anafundisha vitu vitakavyokuwa vimepitwa na wakati ambazo haziwezi kutatua changamoto zilizopo mbele yao.
Prof.Katundu amesema Chuo hicho kimekuwa muhimu kwa taifa katika ufundishaji na uzalishaji wa wataalamu wa sekta ya maji.
Aidha amesema serikali imekuwa ikielekeza vijana wapewe kipaumbele katika taasisi zetu kwaajili ya mafunzo ya vitendo,tunamamlaka ya kutosha zilizopo chini ya Wizara yet, naomba Mkuu wa Chuo kuweka utaratibu ambao utaratibiwa vizuri kuhakikisha vijana wanaohitimu pale panapokuwa na fursa wanahakikisha wanapata mafunzo kwa vitendo,”amesema na kuongeza
“Serikali inajenga mazingira wezeshi ya ajira lakini ajira tunatengeneza wote sekta binafsi na serikali,vijana wakipata mafunzo ya vitendo wanapata umahiri wa kuweza kujitegemea katika kazi zao za ujasiriamali kazi za maji zipo kila siku,”amesema.
Kwa Upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Maji,Dkt Felician Komu, amesema kila mwaka ndani ya kipindi cha miaka mitano chuo chao kimeweza kuzalisha wastani wa vijana 450 wa Astashahada, Stashahada,Shahada ambao ni wataalamu mahiri wanaohitajika katika sekta ya maji.
Amsema Chuo kinachangia maendelezo endelevu kwa taifa kwa kuzalisha wataalamu wa maji nchini.”Chuo kimeendelea kuongeza programu za mafunzo kwendana na changamoto ya kisekta hadi sasa programu 14 za ngazi ya Cheti,Diploma na Degree zinatolewa na chuo hicho”amesema.
Amesema kwa mwaka ujao chuo kinakamilisha na kuanza kutoa mafunzo ya programu mpya ambazo zinatarajiwa kuwa programu 13 katika ngazi ya Stashada na Shahada ya uvamivu ili kutatua changamoto za kisekta.
More Stories
Nani kuwa mrithi wa Kinana CCM?
Watendaji Songwe wapatiwa mafunzo uboreshaji daftari la mpiga kura
Samia: Mwaka 2024 ulikuwa wa mafanikio