Na Rose Itono,TimesMajira Online, Dar
UONGOZI WA Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere umesema miradi ya ubunifu iliyobuniwa na wanafunzi wake itasaidia kutatua changamoto mbalimbaki zinazoikabili jamii.
Akizungumza kwenye maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Dar es Salaam jana Mratibu wa mafunzo ya Shahada za Awali chuoni hapo Dkt.Samwel Lunyelele amesema chuo kinajivunia bunifu mbalimbal za wanafunzi wake ikiwepo ya malipo ya maji kabla ya kutumia.
Dkt.Lunyelele amesema chuo kimezalisha wabunifu mbalimbali ambao watasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii
Akizungumzia ubunifu wake Jumbe Kambaya ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho aliyebuni mita ya maji ya malipo kabla alisema mita hiyo itamuwezesha mtumiaji kulipia maji kupitia mitandao ya simu kabla ya kutumia na kisha atapokea namba (token) kutoka kampuni husika na kisha kuingiza namba aluzotumiwa katika mita yake kwa kutuma ujumbe kwenye namba ya mita yake
Ameongeza kuwa utumiaji wa njia hiyo utapunguza malalamiko ya juu ya usomaji wa mita.
Naye Peter Mwakalesya mwanafunzi mwingine wa chuo hicho aliyebuni ubao unaofuta wenyewe amesema ubao huo utatatua tatizo la walimu kutumia nguvu nyingi na kuwapunguzia muda.
“Walimu wanatumia nguvu nyingi katika kufuta ubao na kupoteza Musa mwingi, “amesema Mwakalesya.
Amezitaja faida za ubao huo kuwa mbali na kupunguza muda pia zitawapunguzia walimu aza mbalimbali za kiafya wanazokutana nazo walimu kwa ufutaji ubao.
More Stories
Wafanyabiashara wakutana Dar,kujadili hali ya biashara
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo