Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya
WILAYA ya Chunya Mkoani Mbeya ni miongoni mwa miji 28 nchini itakayonufaika na mradi wa maji kupitia benki ya Exim ya India ambapo jumla ya shilingi Bil.13 zitatumika kutekeleza mradi wa maji kutoka mto Gwaziva ulioko Kata ya Ileya Wilaya ya Mbeya vijijini.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amefika katika chanzo hicho na kuridhishwa na wingi wa maji kwa mwaka mzima uliopo katika chanzo hicho.
Amesema kuwa kuwa wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuruhusu fedha nyingi kutumika kwenye miradi ya maji jambo ambalo litaketa faraja kwa wananchi.
“Kama mradi huu wa Miji 28 kwa wilaya ya Chunya zaidi ya Bil.13 zinatarajiwa kutumika na tayari fedha zipo hili Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kutatuta fedha kupitia benki ya Exam nchini India na kama mnakumbuka tulisaini mikataba na wakandarasi wote pale Ikulu Chamwino”amesema Mhandisi Mahundi.
Hata hivyo Mhandisi Mahundi ametoa wito kwa wakurugenzi wa Mamlaka za maji nchini na wakala wa maji vijijini( RUWASA)kutokuwa wavivu kutafuta vyanzo vya maji ambavyo vitapelekea miradi kuwa endelevu.
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwataka Mameneja wa Mamlaka za maji na wakala wa maji vijijini ( RUWASA )nchini kutafuta vyanzo vya maji ili kutatua kero za maji.
Katika hatua nyingine Mahundi amesema chanzo hicho kitawezesha upatikanaji wa maji kwa gharama nafuu zaidi kwani yatasafiri kwa mselekeko kwa zaidi ya kilomita 36 kufika Chunya Mjini.
Mhandisi Ndele Mengo ni Mkurugenzi wa ufundi wa wakala wa Maji vijijini (RUWASA )amesema Wilaya ya Chunya ina vyanzo vichache vya maji na maeneo mengine hupata maji ya visima ambayo yana magadi na hutumia kwa kufulia tu si kunywa.
Ndele amesema mradi huo utanufaisha vijijini vinavyopitiwa na mabomba katika Kata za Kiwanja na Mbugani na kwamba maji katika mto huo hayana magadi na ni salama kwa watumiaji.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa mamlaka ya Maji Chunya Francis Mwampashi amesema miradi utajengwa chanzo cha maji Cha mto Gwaziva.
Amesema kuwa wilaya ya chunya
mjini mahitaji ya uzalishaji maji kwa siku ni milimita 1,080 na kwamba kuna upungufu wa asilimia 57 ya mahitaji ya maji kwa siku.
More Stories
Dkt.Mathayo:Dkt.Samia,Dkt.Mwinyi wanastahili,ajivunia mafanikio jimboni
Wanafunzi 3000 wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Rais Samia, Mwinyi ‘mitano tena’ Nchimbi aula