Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mapema leo asubuhi, tayari kuelekea jijini Arusha kufanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumamosi ya Julai 22,2023.
Akiwa ameambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Stephen Wassira na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Ndugu Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu Chongolo baada ya kuwasili uwanja wa ndege, amelakiwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Katika mkutano huo wa leo, pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu Chongolo ataelezea hatua kwa hatua usahihi wa makubaliano ya uwekezaji kwa ajili ya kuboresha uendeshaji na ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam, lengo likiwa kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma kwa viwango vya hali ya juu tofauti, ili kuongeza, tofauti na ilivyo sasa.
More Stories
Dodoma yaandaa Kongamano kutatua changamoto za ajira kwa vijana
Dkt. Pindi Chana aweka jiwe lamsingi jengo la jiolojia Karatu
TotalEnergies yampongeza Rais Samia maboresho kwenye elimu