November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chawa wa Mama Ilala wampongeza IGP Wambura

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

CHAWA wa Mama Wilaya ya Ilala (CHAMATA) wamelipongeza Jeshi la Polisi nchini pamoja na Inspekta Jenerali Camilius Wambura, kwa kuzuia maandamano na vikundi vya ghasia vyenye nia ovu ambavyo vilikuwa vinataka kuhatarisha amani ya nchi.

Tamko hilo la kulipongeza Jeshi la Polisi nchini limetolewa na Katibu wa Chawa wa Mama Wilaya ya Ilala CHAMATA Said Tekelo ,wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari .

“Ndugu zangu waandishi wa habari Rais amezidi kujipambanua kitaifa na kimataifa kuwa yeye ni mwanademokrasia ,Sasa tunaruhusu Demokrasia nchini isiwe chanzo cha wahuni wachache kutumia uhuru huo kuhatarisha amani ya nchi yetu tunalipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kung’amua nia hiyo ovu” alisema Tekelo

Katibu wa CHAMATA Wilaya ya Ilala Tekelo amesema chawa wa mama Ilala wanamvaa mtu yoyote atakayemvaa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumjibu kwa hoja Ili kuendelea kumtia moyo Raiswa juhudi anazozifanya za kuleta maendeleo ya nchi na kuleta fursa za kiuchumi katika Tanzania ya viwanda na Biashara .

Saidi Tekelo amesema
kwa sasa Taifa letu linapiga hatua kubwa kutokana na uongozi mahiri wa Rais Shupavu asiyekuwa na upendeleo nyanja za kisiasa ,Kidini,Wala kikanda ambapo anafanya Maendeleo kote kote nchini kwa kiasi kikubwa na weledi wa hali ya juu.

Wakati huohuo chawa wa Mama Ilala wamelipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Tulia Ackson kupitisha kwa kauli Moja juu uwekezaji wa Bandari ya Tanzania ambapo uwekezaji wa Bandari hiyo utakuwa na tija kwa Taifa na kizazi cha sasa na baadae .

Aidha pia wamempongeza Katibu Mkuu wa chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Daniel Chongolo na Viongozi wa chama hicho kufanya ziara nchi nzima kutoa elimu kuhusiana na masuala ya uwekezaji huo kwa kutoa elimu kwa Watanzania ya kutosha kuhusiana na suala hilo ikiwa tofauti na wahuni wachache walipokuwa wanataka kupotosha dhamira njema na halisi ya uwekezaji huo