July 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chatanda awataka wanawake kutumia nishati salama,kulinda afya zao

Na Patrick Mabula , Kahama.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake CCM (UWT) , Mary Chatanda amewataka akinamama kupitia matokeo hamasika kutumia nishati salama gesi na kuondokana na matumizi ya kuni , kulinda afya zao.

Wito huo ametoa juzi kwa viongozi wa UWT ,toka kata zote 130 za mkoa wa Shinynaga wakiwemo wa Serikali , Madiwani , makundi maalumu ya watu wenye ulemavu katika mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022

Akiongea nao amesema matokeo ya Sensa ya wat una makazi yanapaswa kuwafikia watu wote ambapo aliwataka wanawake kuyatumia katika maendeleo yao ikiwemo kutumia nishati salama ya gesi kupikia na kuondokana na kuni kwa sababu wamekuwa wakiathirika na moshi.

Chatanda amesema matokeo ya Sensa ya watu na makazi ni muhimu sana na katika kupanga mipango ya maendeleo na kutatua changamoto za wananchi na kuwahamasisha wanawake kutumia nishati salama ya gesi kupikia ili kutunza mazingira.

“ Matoke hayo yawasaidie wanawake katika kujenga hoja mbalimbali za maendeleo kwenye nyaja zote katika maeneo yao kwa kufaata matakwa ya watu wa maeneo wanayoishi ,”amesema Mwenyekiti wa Taifa wa UWT , Chatanda.

Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Shinyanga , Santiel Kirumba ameiomba Serikali kupunguza gharama ya kununua gesi ambayo ipo juu kutakakowasaidia wanawake kununua nishati hiyo kwa matumizi ya kupikia na kuondokana na matumizi ya kuni kutokana na kuteseka na moshi.