December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chanjo ya Surua-rubella kutolewa Dar es Salaam

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

SERIKALI ya mkoa wa Dar es salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na wadau mbalimbali wa maendeleo wamepanga kutoa chanjo ya surua rubella kwa watoto wenye umri wa miaka miwili na miezi minne ili kulinda afya za wananchi hasa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

katika zoezi hilo litaanza kwa uhamasishaji kwenye jamii kwa kutumia vipaza sauti mita kwa mitaa na kuwatumia watoa huduma ngazi ya jamii (CHWs) siku moja kabla ya kuanza huduma hiyo itakayofanyika kwa muda wa siku tano kuanzia feburuari 1, mpaka feburuari 5,2023.

Akizungumza na waandishi wa habari leo january 26, 2023 jijini Dar es Salamm katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam Rehema Madenge, amesema kuwa lengo la utoaji wa chanjo hiyo ni kuwafikia watoto takribani 156,193 kwa dozi zote mbili za surua rubela.

“ni matarajio ya mkoa kwamba zoezi hili litachangia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo ya mkoa ya mwaka kwa kuchanja watoto wapatao 156,193 na chanjo hizi zitatolewa kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma za chanjo katika mkoa wa Dar es salaam kwa watoto chini ya umri wa miaka miwili kwa ajili ya chanjo ya surua” amesema Madenge

Hivyo, Madenge amesisitiza wazazi na walezi wote wenye watoto wa umri uliyotajwa kuwapeleka kupata chanjo ya surua-rubela kwa sababu kwa mtoto asiyepata chanjo hiyo ni hatari kwa afya yake na kwa jamii inayomzunguka.