Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka Kampuni ya magari ya inchcape automotive Tanzania kulipa Kodi kwa wakati ni nyenzo muhimu katika biashara.
Akizungumza hayo jijini katika hafla ya uzinduzi wa magari mapya kwenye soko la Tanzania lililofanywa na Kampuni hivyo ambapo amesema uwekezaji wenye tija unaendana na ulipaji wa Kodi.
“Tunawapongezeni sana inchcape automotive Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wa uuzaji magari bei nafuu hivyo kwa kiwango hiki uwekezaji unaendana na ulipaji wa Kodi,”amesema Chalamila
Chalamila ameeleza kuwa uwekezaji huo ufungue milango ya fursa za utoaji wa ajira kwa watanzania lakini waongeze ufanisi katika utoaji wa huduma hapa nchini.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Kampuni hiyo Alfage Mnangwa amesema kuanzishwa kwa Changan tanzania ni uthibitisho wa Imani katika uhusiano kati ya China na Tanzania.
Hata hivyo ni muhimu soko la Tanzania na wateja katika mazingira ya kimataifa, changan tafsiri yake ni usalama wa kudumu ikionyesha ahadi kuu ya Kampuni na kijitolea kwa utafiti na maendeleo.
Mnangwa amesema kuwa magari yote yanakuja yakiwa na injini zenye mifumo wa Euro 6 na Euro 4 zikiwa na dhamana ya kuanzia miaka miaka 3 hadi 5 kulingana na toleo.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja