December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chalamila akubali kuilea DCPC

Na Rose Itono, timesmajira

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Charamila  amekubali kuwa mlezi wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam DCPC

Akizungumza na wanachama wa Klabu hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa waandishi wa Habari na Wadau  Jana amesema yuko tayari kuilea DCPC na kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo

Amesema waandishi wa habari ni muhimu katika kuhabarisha umma hivyo kwa kuzingatia hilo kuna kila sababu ya kushirikiana nao kwa karibu kwa kushauriana na kuangalia namna ya kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa kitovu cha kuigwa na majiji mengine.