Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Kituo cha uzazi cha Chennai (CFC) kimewataka wananchi waliokosa watoto kujitokeza na kupata huduma zao ambazo zitawasaidia kuondokanana na changamoto hiyo ya uzazi kupitia huduma yao ya upandikizaji wa mimba (IVF).
Kutokana na uzoefu na ujuzi wa muda mrefu ambao wamekuwa nao, hadi sasa Kituo hicho kimeshahudumia watanzania 500 ambao tayari wamefanikiwa kupata mimba lakini pia zaidi ya watu 500,000 ulimwenguni wamepata huduma hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya matibabu na Afya (24th mediexpo Afrika), Mwenyekiti na Mkurugenzi wa CFC, Dkt. V M Thomas amesema huduma ya ushauri wa hatua kwa hatua kwa mama mwenye changamoto ya uzazi inatolewa bure katika maonesho hayo ambayo yameanza Agost 29 na kumalizika Agosti 31 mwaka huu.
“Katika maonesho haya ya mwaka 2024 tupo kwa siku tatu, na tunatoa ushauri wa bure kwa mtu yoyote ambaye angetamani kuwa mzazi”
“Kituo chetu kinakuhakikishia kwamba kwa ujuzi tulionao, kwa asilimia 90 tunaweza kukusaidia na kupata mtoto” Amesisitiza
Dkt. Thomas amesema kituo hicho kina vifaa vya maabara vya kati kwa wataalam wote wa IVF ambapo wagonjwa wote wataweza kutibiwa katika mazingira ya kiwango cha juu.
Aidha amesema kupitia kituo hicho , wanaendelea kufanya mazungumzo na Wizara ya Afya nchini ili huduma hiyo iweze kuwepo hapa Tanzania.
Mbali na hayo, Daktari huyo alisema wanafanya jitihada ili waweze kuwafikia watu wengi zaidi hasa kwa kushiriki maonesho mbalimbali,mitandao ya kijamii, vyombo vya Habari kwa kuwapa elimu na huduma hiyo kwa ujumla.
Naye mmoja wa washiriki aliyehudhuria maonesho hayo, John Joel alisema kuwa fursa ya upandikizaji mimna kwa wanawake itasaidia sana hasa katika kupunguza gharama za matibabu kwa watanzania wanaosafiri kupata matibabu hayo nje.
More Stories
Tanzania kuwa mwenyeji Mkutano wa Kimataifa matumizi bora ya Nishati
Madiwani Ilala watoa chakula kwa watoto yatima
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa