September 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yasisitiza kauli ya Rais, kifo cha mjumbe CHADEMA

Na Penina Malundo,Timesmajira

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM),kimeunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha uchaguzi wa kifo cha Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Ali Kibao kufanyika kwa haraka na hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Pia wamesema watanzania wanawajibu wa kuacha kunyoosheana kidole bali kuacha uchunguzi wa kweli na wakina kufanyika kwa haraka.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na wahariri pamoja na waandishi wa habari juu ya Kifo cha Mjumbe huyo wa CHADEMA,Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt.Emmanuel Nchimbi alisema Rais Samia ametoa kauli ya wazi kwa tukio hilo lilitokea na amekerwa nalo.

Amesema CCM imekasirishwa na tukio hilo hibyo wameitaka Serikali kuharakisha uchunguzi huo kutolewa kwa haraka na matukio ya namna hii yakomeshwe.

“Nilipopata taarifa hii,Mbowe alinipigia simu kama mara tano nilijua angeniambia habari ya msiba imekuaje,ila ujasiri wa kupokea simu ile sikuwa nayo na baadae nilimwandikia meseji ya kumuomba radhi jambo lile lilinivuruga nikashindwa kupokea simu.

“Pia tunasisitiza kwamba wananchi wa Tanzania kutoa muda wa kufanya uchunguzi kuhakikisha kwamba maamuzi tunayoyafanya yanatenda haki,”amesema na kuongeza

“Juzi mliona tukio la Geita watu waliona wanaume wawili wanapita na watoto mmoja akiwa na mwaka mmoja na mwingine akiwa na miaka mitatu walipofika karibu na mnada watu waliwakimbiza na kudai kuwa wezi wa watoto,walipofika kituo cha polisi waliingia ndani wananchi wakanza kushambulia kituo cha polisi ambapo polisi waliamua kutumia silaha kuwazuia kuwachukua lakini nini kilibainika kumbe mmoja kati ya wale ni Mzazi wa watoto na mwingine ni shemeji ake na walitoka kuwachukua watoto kwa Bibi yao na wanarudi nyumbani kwao,”ameelezea.

Amesema lazima kama taifa kufanya kila njia kuhakikisha raia wote wanatendewa haki na kuhakikisha mtu yoyote anayetuumiwa anakosa asionekane na kosa hadi uthibitisho utakapotolewa.

“Na sisi kama CCM tutafanya kila itakayowezekana Demokrasia katika nchi yetu iendelee kushamiri nchini,mahusiano ya vyama na vyama yaendelee kuimarika na nchi yetu tuijenge,”amesema na kuongeza

“Naamini kwa dhati kubwa nchi hii ni ya watanzania wote wanawajibu wa kipekee kuijenga nchi yetu kwa kujua tumerithishwa taifa zuri na waasisi wetu na tunawajibu wa kipekee kuhakikisha watoto na wajukuu wetu wanapata taifa zuri,”amesema.

Amewaomba viongozi wakisiasa wengine kuendelea kushirikiana kwani CCM inaamini katika mazungumzo, ushirikiano kati yao na wao kwani wanawajibu wa kujenga taifa la umoja na ushirikiano ili kuwa na taifa tulivu.

Amesema jambola hovyo ni ikifikia mahali wananchi wanakuwa na hofu na mashaka juu ya nchi yao,tushirikiane na kuwakumbusha raia kuwa kila Mtanzania anawajibu wa kumlinda mtanzania mwenzake na anawajibu wa usalma wake na mwenzake.

***Akizungumzia kuhusu Jeshi la Polisi kufarakanishwa na wananchi

Dk.Nchimbi amesema kumekuwa na jitihada kubwa za kufarakanisha Jeshi la Polisi na wananchi na kwamba katika ziara wanashuhudia wananchi wanajenga vituo na wanachoomba ni kupatiwa askari, hivyo haikubaliki kuona matukio machache yakitaka kuharibu sifa nzima ya jeshi la polisi.

Amesema kuwa kati ya mwaka 2017 hadi mwaka 2023, Polisi ambao wameuawa katika matukio ya yaliyohusisha majambazi na kuongeza jumla ya polisi 141 wamejeruhiwa.

“Hawa polisi ambao zinafanyika jitihada ambazo zinataka kuonesha Polisi hawafai, polisi wakae dakika 24 tu tuone nini kitakachotokea.

***Akizungumza kuhusu watu waliopotea

Dk.Nchimbi amesema watu waliopotea katika kipindi cha miaka mitano ni 151 na waliopatikana 141 kwa jitihada za Polisi.“Kwa hiyo kama kuna jambo ambalo halitasaidia nchi yetu ni kuwafarakanisha Polisi na wananchi kwa hiyo ni vema tukaacha kunyooshena vidole.

“Tunaye Rais anayeishi kwa vitendo maridhiano, umoja na mshikamano. watanzania wote ni ndugu na tunakila sababu ya kushirikiana kujenga nchi.”amesisitiza.