January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yawakabidhi ng’ombe Klabu ya Yanga

Mwandishi wetu, Timesmajira online

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM ) kupitia Idala ya Itikadi na uenezi kimekabidhi Ngombe watano Kwa klabu ya Yanga na Ngombe mmoja wa klabu ya Simba ikiwa ni kutimiza ahadi ya Mkuu wa idala ya Itikadi na uenezi Paul Makonda aliyoitoa siku chache kabla ya mchezo wa watani wa jadi.

Akikabidhi Ngombe hao Kwa viongozi wa Klabu ya Yanga Jijini Dar es salaam Novemba 24 kwaniaba ya Mkuu wa idala ya Itikadi na uenezi Paul Makonda, katibu msaindizi Mkuu wa idala hiyo, Shaibu Akwilimbe amesema CCM kupitia Idala ya Itikadi na uenezi imekuja kutekekeleza ahadi yake ambayo iliitoa siku chache kabla ya mchezo wa watani wa jadi.

Amesema katika kuhamasisha michezo Mkuu wa Idala ya Itikadi na uenezi Paul Makonda aliwahidi Kila goli atatoa zawad ya Ngombe.

“Kwasababu ahadi ilikuwa Kila goli Ngombe mmoja nmekuja Kwa niaba yake kukabidhi Ngombe hawa watano Kwa viongozi wa yanga na mmoja Kwa klabu ya Simba”amesema

Akizungumza kwa niaba ya wazee wa Yanga, Mohamed Msumi alikishukuru Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kutekekeleza ahadi yake na kueleza kuwa hiyo imedhiirisha Chama hicho kinafata misingi sahihi kwani michezo ni burudani.

“Chama Cha Mapinduzi CCM kimetimiza ahadi ya na wamefanya ilani ya Chama Cha Mapinduzi yenye sera ya michezo”amesema

Nakuongeza kuwa
“Goli hizi tato zimekuwa mpatanishi Kwa watani wa watani wetu wa jadi bila kuwapiga tano wasigejua wanamapugufu Gani”amesema Msumi

Aidha aliiomba klabu ya Simba kufuata mawazo na maoni ya wazee wao kama uongozi wa yanga unavyothamini wazee wake