July 1, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yaridhishwa na ujenzi miradi sita ya maendeleo Igunga

Na Lubango Mleka, TimesMajira Online – Igunga

KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora imafenya ziara ya kukagua ujenzi wa miradi Sita ya maendeleo inayotekelezwa wilayani hapa na kulidhishwa na hatua zilizofikiwa katika miradi hiyo ambayo inaghalimu kiasi cha shilingi Bilioni 22 kati ya Bilioni 80 ambayo Wilaya ya Igunga imepokea kutoka Serikalini.

Miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ya Siasa ya CCM wilaya ya Igunga ni pamoja na ujenzi wa madarasa matano na ofisi mbili za walimu Shule ya Sekondari Ziba iliyopo kata ya Ziba, ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 1,000,000 lilipo mlima wa Bulenya kijiji cha Igogo litakalo hudumia vijiji 18 na unasimamiwa na RUWASA, ujenzi wa miundombinu ya kutibu majitaka na topetaka unaosimamiwa na IGUWASA uliopo katika kitongoji cha Mwalugala kata ya Igunga.

Miradi mingine ni ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la kuhifadhia maiti, wodi ya wanaume na jengo la mionzi katika hospitali ya wilaya ya Igunga, ujenzi wa uziona bweni lenye kulaza watoto 80 wenye uhitaji maalumu katika shule ya msingi Igunga na mradi wa umeme utakao sambazwa na TANESCO Igunga katika migodi wenye thamani ya shilingi bilioni 2.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa shule ya Sekondari Ziba kwa kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Igunga, Mwalimu Mkuu Ally Nohoye alisema kuwa mradi huo wa ujenzi wa ujenzi wa madarasa matano na ofisi mbili za walimu umegharimu kiasi cha shilingi milioni 330 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Naye Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Igunga John Wambura Wangwe, amesema kuwa upanuzi wa maradi wa maji ya Ziwa Victoria kutoka Igogo kwenda Igurubi utakao hudumia vijiji 18 na wananchi 79,854 watanufaika na mradi huo, ambao unahusisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 1,000,000, ujenzi wa vituo 57 vya kuchotea maji, kuchimba, kulaza na kufukia bomba kilometa 150.

“Mradi huu ni wa miezi 28 ambao umeanza kutekelezwa ujenzi wake kuanzia tarehe 28.10.2023 na tunatarajia utakamilika tarehe 28.10.2024, na kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa tanki kule mlima wa Bulenya ambalo lipo katika asilimia 78, tumechimba mtaro mita 48,184, kuunga bomba, kulaza na kufukia mita 44,000, utengenezaji wa barabara kuelekea eneo la ujenzi wa tanki na ujenzi wa vituo 18 vya kuchotea maji, na mradi wote umefikia asilima 56, na thamani ya mradi wote ni bilioni 20.

Huku Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Igunga Mjini (IGUWASA) Mhandisi Hamphrey Mwiyombela akisema kuwa ujenzi wa bwawa la kutibu majitaka na topetaka utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.8 na unatekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji.

Mradi huo utahusisha ununuzi wa magari mawili ya kunyonyea majitaka moja lenye uwezo kunyonya lita 10,000 na jingine lita 5,000 na utahudumia watu 82,768 na umeanza kutekelezwa mwezi Julai, 2023 na unatarajiwa kukamilika Octoba, 2024 na umefikia asilimia 23. 5.

Kamati hiyo pia imetembelea mradi wa upanuzi wa hospitali ya wilaya ya Igunga ambapo Mganga Mfawizi Melchedes Magongo amesema kuwa wamepokea kiasi cha shilingi milioni 900 kutoka Serikalini na utahusisha ujenzi wa majengo manne, jengo la wagonjwa wa nje (OPD) linalogharimu kiasi cha shilingi milioni 447.

Jengo la kuhifadhia maiti litaghalimu kiasi cha shilingi milioni132, jengo la mionzi linagharimu kiasi cha shilingi 221 na wodi ya wanaume itagharimu shilingi milioni 93 na umeanza ujenzi wake mwezi Machi, 2024 na utakamilika mwezi Agosti, 2024.

Katika Mradi wa ujenzi wa uzio na bweni la wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika shule ya msingi Igunga, Mwalimu Mkuu Sofia Mnyeto amlisema kuwa, ” Shule ya Msingi Igunga ilipokea kiasi cha shilingi milioni 80 kutoka Serikalini kupitia kampeni ya UVIKO-19 mwezi Octoba 2021 kwa ajili ya ujenzi wa bweni lenye kubeba wa wanafunzi 80 na ujenzi bado unaendelea kama mnavyoona,”

Akizungumza kwa niaba ya kamati ya Siasa ya CCM, Katibu wa CCM wilaya ya Igunga Ebenezer Emannuel amesema kuwa, wao kama Chama cha Mapinduzi na wilaya ya Igunga wamekuwa wakitekelez majukumu mengi yanayohusu Chama, ya kikatiba na kikanunu ikiwa ni pamoja na kukisimamia Chama kuanzia ngazi ya wilaya, kata hadi shina ambapo wametembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa lengo la kuhabarisha umma juu ya mambo mazuri yanayo tekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Huku Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Igunga Peter Oronge Kalindo akiwataka wahandisi wa halmashauri ya Igunga na wasimamizi wote wa miradi hiyo kuisimamia vyema na kuhakikisha kasoro ndogondogo ambazo zimejitoke katika baadhi ya miradi zinarekebishwa na kukamirisha miradi hiyo kama mikataba ilivyo sainiwa.

Wajumbe wa kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Igunga wakipata maelezo juu ya ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 1,000,000 lililopo Mlima bulenya ambalo litahudumia vijiji 18 wilayani hapa litakapi kamilika kutoka kwa Kaimu Meneja wa RUWASA John Wangwe Chacha.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi John Wangwe Chacha wa kwanza kushoto akitoaa taarifa ya ujenzi wa tanki la maji leenye ujazo wa lita 1,000,000 lililopo Mlima bulenya ambalo litahudumia vijiji 18 wilayani hapa.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Igunga mkoani Tabora Mafunda Ntemanya wapili kutoka kushoto akimsikiliza Mganga Mfawizi wa Hospitali ya wilaya ya Igunga Melchedes Byabato Magongo alipokuwa akielezea hatua iliyofikiwa katika upanuzi wa mradi wa ujenzi wa majengo manne katika hospitali hiyo.
Jengo jipya la bweni na uzio la wanafunzi wenye uhitaji maalumu Shule Msingi Igunga ambalo limetembelewa na kukaguliwa na kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Igunga.