September 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yaingilia kati, uchaguzi Kibaha Mjini

Na Penina Malundo, Timesmajira 

CHAMA cha Mapinduzi CCM,  kimeagiza 

 kurudiwa kwa uchaguzi wa kumpata Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha Mjini.

Akitoa maelekezo hayo jana wilayani Masasi mkoani Mtwara ,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza  viongozi wa chama hicho wa  wilayani hiyo.

Amesema julai 27, mwaka huu kilifanyika kikao cha CCM cha madiwani Kibaha Mjini kwa lengo la kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha Mjini ambapo majina yaliyopelekwa  kwenye kikao cha Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani lilikuwa  jina moja lililorudishwa  kwa ajili ya kupigiwa kura.

“Kuna sehemu wamegombea Kibaha Mjini, nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri wamegombea watu wawili, jina likarudi moja, kura za ndiyo zikapigwa sita na kura za hapana  zilipigwa 11. Ugomvi wa nini? Na ndiyo uamuzi wa mwisho,”amesema na kuongeza 

“Kuna ugomvi hapo kwani? Wameniuliza Katibu Mkuu tunaomba maelekezo yako. Maelekezo gani mnayataka?, rudieni uchaguzi. Ngoma imeshakataliwa hiyo.huyo ameshakataliwa wasitafute mchawi”.amesema.