Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Pemba
MKUTANO wa kampeni wa mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi umehudhuriwa na umati wa wanachama wa CCM katika Jimbo la Kiwani Wilaya Mkoa Mkoa Kusini Pemba.
Kufikia saa tano asubuhi Uwanja wa Kiwani ulisheheni wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla ambao wemefika kusikikiza ilani, sera na mwelekeo wenye kuleta matumaini kwa wananchi.
Kujitokeza kwa wingi kwa wananchi katika mkutano huu ni ishara tosha ya kuendelea kukubalika kwa Chama Cha Mapinduzi na kwamba ushindi wa CCM hauna shaka yoyote.
” Kwa miaka mingi sijapata kuona watu wengi kama hawa… hii ni ishara ya kukubalika kwa mgombea wetu Dk Hussein Mwinyi na Chama chetu,” anasema Hamad Said Faki Mkaazi wa Kiwani.
Mgeni rasmi katika mkutano huo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Viongozi mbalimbali wa CCM.
More Stories
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Maandalizi ya mkutano mkuu CCM yapamba moto