November 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM vingunguti wadondosha Mbuyu wa CHADEMA

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

CHAMA cha MAPINDUZI CCM kata ya Vingunguti wilayani Ilala ,kimeangusha Mbuyu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kufuatia aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Vingunguti DAVID ANSELIM PAUL kujiunga na Chama Tawala cha Mapinduzi katika mkutano wa hadhara.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) DAVID PAUL alijiunga na chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama ambayo imewasilishwa na Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ,ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti.

Akizungumza katika mkutano huo mara baada kuvishwa magwanda ya CCM DAVID PAUL alisema anashukuru kurejea Chama cha Mapinduzi CCM atapigania CCM iweze kushinda kwa nguvu zake zote ili iweze kushika dola ccm ni Taasisi kubwa.

“Naunga mkono juhudi za chama cha Mapinduzi CCM kuanzia sasa ili kuakikisha ccm ina shika dola nitatumia nguvu zangu zote “alisema David.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu wa CCM wilaya ya Ilala Sylverter Yared ,alisema kurudi kwake CCM David Paul awe sehemu Salama CCM ina viongozi imara kata ya Vingunguti ina fanya siasa safi.

” CCM chama chetu kina Demokrasia leo wamempa kadi ya CCM DAVID PAUL yupo sawa na watu wengine waliopo CCM hivyo usiwe na wasiwasi utashirikiana na chama katika shughuli mbalimbali “alisema Yared.

Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto akiwasilisha Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM alieleza baadhi ya mambo mbali mbali aliyotekeleza ikiweko sekta ya afya alisema shule ya Kombo ina jengwa madarasa 11 kwa shilingi milioni 158 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan dhumuni shule hiyo iwe nzuri .

Meya Kumbilamoto alisema shule ya Msingi Mtakuja ya kisasa Dkt Samia Suluhu Hassan amejenga madarasa 13 na vyoo 20 na shule ya Msingi Vingunguti inajengwa madarasa 16 kwa sasa sekta ya Elimu wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Dkt samia suluhu Hassan imefanya mambo makubwa .

Akizungumzia miundombinu ya Barabara alisema Vingunguti zinajengwa Barabara za kisasa na Mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP ambapo pia zitafungwa taa za kisasa hivyo wananchi wavute subira Vingunguti itakuwa kama ulaya.