Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitatoa makatapila 20 kwa ajili ya kuboresha barabara zilizopo Bunju mkoani Dar es Salaam.
Pia kimesema hakiwezi kumbeba kiongozi yoyote endepo hafanyi kazi ya utekelezaji wa ilani ikiwemo kutatua changamoto za Wananchi kwasababu misingi ya chama hicho ni kutatua kero na mateso ya wananchi.
Hayo yamesemwa Jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi , Uenezi na Mafunzi, Paul Makonda akiwa Bunju Jijini Dar es Salaam wakati alipoanza ziara yake ya mikoa 10 yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
“Nitamletea katapila 20 kwa muda wa wiki nzima katika Jimbo lake, na hizo katapila ninamkabidhi mtu wa TARURA ambapo hadi kufikia Jumanne ya wiki ijayo nataka nione katapila zimegawana mitaa kwaajili ya kurekebisha barabara zote za Jimbo la Kawe ambazo zinachangamoto,” amesema Makonda.
Amesema chama kimefanya hivyo kwasababu Mbunge wa Jimbo hilo, Askofu Josephat alionyesha dhamira ya dhati ya kuboresha bararaba katika jimbo hilo.
Makonda amesema chama hicho akitakubali kubeba watu katika kipindi cha uchaguzi.
“Mwaka huu 2024/25 tutawapima wabunge, wawakilishi pamoja na madiwani namna gani wanatatua changamoto za wananchi wao na jinsi gani wako mstari wa mbele kukijenga chama chao,” alisema.
Ameeleza kuwa viongozi hawana haki kama hawatatui kero za wananchi kwasababu ni jukumu leo kuhakikisha wanapunguza maumivu ya wananchi.
“Kama kuna Mbunge, Diwani, au Baraza la wawakilishi au Wabunge kwa kauli moja tutakupima kwa kazi, si kwa maneno, kugawa kanga katika kipindi cha uchaguzi na kuwarubuni wajumbe, kujipendekeza kwa viongozi,” alisema.
Amebainisha kuwa kazi ya mbunge ni kupambania mgawanyo wa keki ya Taifa na endapo ukiona mbunge amechukua hatua ya ziada ya kutoa pesa za kwake maana yake hayo ni mapenzi yake zaidi kwa wananchi waliompigia kura.
“Kazi kubwa zaidi ya mbunge ni kuhakikisha ile keki ya Taifa wanapokaa Dodoma kwenye bajeti, anapambania Jimbo lake hivyo wabunge wote wanatakiwa wafanye mkutano kabla ya kwenda bungeni, kukaa na wananchi wanaowaongoza kujua changamoto zao ili wakifika kule waongeze sauti,” amesema.
Mbali na hayo, makonda amempigia simu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa na kumtaka afike Bunju baada ya dakika 20 ilikutatua migogoro hiyo.
Amesema duniani kote hawajawahi kumaliza matatizo hata Mataifa makubwa yanayokimbiliwa kuombwa misaada bado yana changamoto.
Amesema changamoto haziwezi kuisha kwa wakati mmoja kwasababu zitaendelea kuwepo kutokana na idadi ya watu katika nchi na hali ya kiuchumi vinginevyo serikali ingeweza kujenga lami kote.
Pia ameeleza kuwa Rais Samia Samia Suluhu ametoa fedha nyingi kwenye sekta ya elimu, Afya, nakuwekeza nguvu kubwa kwenye sekta ya maji.
Amesema kwenye Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM Taifa walimuhoji Waziri wa Nishati, ambaye ni Naibu Waziri Mkuu aeleze kuhusu upatikanaji wa umeme na jinsi Tanzania itaondoka kwenye mgao wa umeme ili wananchi wafanye shughuli zao.
Ameongeza kuwa dhamira ya serikali na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha nchi inaondokana na changamoto ya ukosefu wa umeme.
“Chama kilihoji suala la kukatika katika kwa umeme kutakwisha lini? Miradi hii mikubwa ya umeme itakamilika lini? lakini Chama kikahoji pia gharama za upatikanaji wa umeme zitakuwa ahueni kwa mazingira yetu?, pia wananchi wataendelea kuunganishiwa umeme na kuhakikisha kwamba vijiji vyote vya Tanzania vinapata umeme?,”
“Waziri alikua na timu yake nzima, wakatupa ahadi ya kwamba mwezi huu na mwezi ujao mitambo ile mikubwa kati ya 8 au 9 inaanza kuunganishwa na kujaribiwa ili tuweze kwenda kwenye njia na ndoto yetu ya matumaini ya kuwa na umeme Megawati 2115,” amesema Makonda.
Awali Makonda alipokuwa katika ofisi za CCM wilaya ya Kinondoni amewashukuru Wazee wa Baraza kwa kutatua changamoto na kero za wananchi.
Amesema “Heshima ya Chama chetu ni kutatua changamoto za watu, tumepewa nafasi na ridhaa maana yake tunanayo majibu ya changamoto walizonazo Wananchi wetu,” alisema Makonda.
Pia, amewataka viongozi na Wananchama kwa ujumla kuimarisha chama kuanzia ngazi za matawi na kata.
Aidha Makonda alibainisha kuwa maadhimisho ya CCM yataanza kufanyiwa sherehe kwenye kila kata.
“Wenyeviti wa kata na Madiwani ndio wenye majukumu ya kuandaa na kila Jumuiya iwe na siku yake ya maadhimisho na lengo ni kuhakikisha maendeleo yote yaliyofanywa kwenye kata yanasemwa ambapo itakuwa chachu ya kuona uhai wa chama na Jumuiya zetu za Chama Cha Mapinduzi,” amesema.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa