Na George Mwigulu,Timesmajiraonline,Katavi.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, Kimekanusha uwepo wa viongozi ndani ya chama hicho kuleta wagombea wa nafasi za ubunge katika majimbo kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwakani 2025.
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Katavi, Idd Kimanta akizungumza na waandishi wa habari Disemba 17,2024 amedai tuhuma zinazoelekezwa kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho kuwa na wagombea wao ni upotoshaji usio kubalika.
Akiwa katika ofisi ya CCM Mkoa wa Katavi, Mbali na kuwaomba wananchama kupuuza upotoshaji huo ametoa onyo kwa baadhi ya makada walioanza harakati za kuonesha nia za kugombea uongozi kwenye nafasi za ubunge na udiwani kabla ya wakati ulio ndani ya taratibu za chama hicho.
Kimanta akizungumzia baadhi ya viongozi kuwa na wagombea wao, amewatoa hofu wanachama wa CCM kuwa jambo hilo halipo na wanapaswa kulipuuza kwa sababu lengo lake si jema.
“Hakuna kiongozi yeyote wa chama anayeleta mgombea kwa ajili ya uchaguzi ujao maana kuna taarifa hizo kwamba fulani analeta wagombea…naomba niwaambie wana CCM wenzangu jambo hilo halipo” Kimanta amesisitiza.
Kwa makada ambao tayari wameanza kujipitisha kwenye majimbo ya uchaguzi amesema wanayo orodha yao tayari ambapo wanapaswa kuheshimu wabunge na madiwani waliopo kwa sasa ili waendelee kufanya kazi za kuwatumikia wananchi.
Kiongozi huyo akiwaomba wanachama kusubiria wakati wa mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama amebainisha kuwa chama kipo makini na kitaendelea kufuatilia mwenendo wa kila kada na uteuzi utakapoanza kuelekea uchaguzi ujao kanuni na taratibu zitazingatiwa.
“Sisi tutasimamia kanuni na taratibu za chama wakati ukifika na tusije tukalauminana kwa hao walionza kujipisha kwa wananchi na wanachama wetu” amesema.
Kuhusu uwepo vuguvugu la joto la uchaguzi na makundi katika baadhi ya Majimbo katika mkoa wa Katavi amesema hiyo ni ishara ya kukua kwa Demokrasia ndani ya chama cha Mapinduzi kwa wananchama kuonyesha nia hiyo kwa kufuata utaratibu.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais