Na Hamisi Miraji, Timesmajira Online
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata 14 wilayani Temeke, kimepongezwa na wanachama wa chama hicho kutoka Zanzibar Wilaya ya Mfenesini kwa mapokezi mazuri waliokutana nayo mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana.
Wanachama hao wa CCM Wilaya ya Mfenesini, Unguja waliwasili jana Asubuhi na kupokelewa na wenyeji wao Jumuiya ya Wazazi CCM Kata 14 Temeke huku kikiwa na ndelemo na vifijo pamoja na kupata burudani ya kutosha.
Akizungumza na majira mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mfenesini, Zanzibar, Kessi Mashaka Ngusa amesema amefurahi sana kwa mapokezi mazuri aliyoyapata jambo ambalo limewapa faraja kubwa kuona Chama Cha Mapinduzi kinazidi kuwa imara
Amesema, lengo la ziara hiyo Dar es Salaa ni kujenga undugu baina ya Watanzania Bara na Visiwani katika kubadilishana uzoefu kuhakikisha CCM inazidi kuwa imara.
“Ujio wetu ni kuunga undugu, leo hii tunafurahi Jumuiya ya Wazazi CCM Kata 14 Temeke imetupokea vizuri lakini lengo Kuu kuona jinsi gani ya kubadilishana uzoefu.
“Kama unavyojua wenzetu wa Tanzania Bara wanafanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani lakini sisi mpaka 2025, hivyo tunaamini tutakuwa tumepa vitu vingi sana katika ujio wetu huu,” amesema Ngusa.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata 14 Temeke, Gogo Mzome amesema amefurahi sana kuona Wanachama wa chama hicho kutoka Zanzibar kuwasili na inaonesha jinsi gani undugu wa kuimarisha chama unashika hatamu.
“Tumefurahi kupokea wageni kutoka Zanzibar kwa ajili ya Ziara ya kichama hii inatoa faraja kubwa jinsi gani ya kuimarisha undugu kama walivyofanya waasisi wetu Mwalimu, Julious Nyerere na Abeid Aman Karume kwa kuutengeneza muungano wetu.
“Lakini pia kunadilisha uzoefu wa kichana ili kila mmoja afahamu mbinu zinazotumika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi hakiwezi kuteteleka katika chaguzi mbalimbali na kuendelea kushika dola,” amesema Gogo Mzome.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri ya Wadi Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini, Kijacho Abdallah Vuai alisema amefurahishwa na mapokezi walioyapata kutoka kwa wenyeji wao.
Amesema, anaamini kama CCM itaendeleza utamaduni huo basi hauka chama kinaweza kushindana nao kutokana na uimara watakaouweka.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CCM Kata 14, Tedy Mgusi Liakwama amesema amefurahi kuona Wazanzibar wakiwasili Dar kwa ajili ziara ya kichama.
Hata hivyo amesema, lengo ya Ziara hiyo ni kudumisha udugu baina ya Watanzania Bara na Visiwani kuhakikisha CCM inapiga hatua pande zote mbili za Muungano.
“Katika kuhakikisha Undugu unaimarika baina yetu hatuna budi kuuenzi Muungano ulioasisiwa na Hayari Mwalimu Nyerere Rais wa kwanza Tanzania Bara na Abeid Aman Karume, hivyo ujio wa wageni wetu utakuwa chachu ya kukijenga Chama Cha Mapinduzi (CCM),” amesema Tedy.
Alitoa wito kwa Jumuiya tatu zilizoo CCM Kata 14, kuanzia vijana, Wazazi na UWT kushirikiana kwa hali na mali kuhakikisha kata hiyo inasimama imara.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM