November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM Ilala yawataka Madiwani kuunda mikutano ya kueleza Ilani

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala kimewataka madiwani na Wenyeviti wa Serikali za mitaa kufanya mikutano ya adhara katika kata zao na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM kazi zilizofanywa na Serikali ikiwemo miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya Ilala Said Sidde,alitoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Pugu ulioandaliwa na CCM kata ya Pugu .

“Nina mpongeza Mwenyekiti wa ccm kata ya Pugu Frank Mangati ,kuandaa mkutano mkubwa wa adhara kuelezea utekelezaji wa Ilani ya ccm katika kata ya Pugu yale yaliotekelezwa na Serikali ya Dkt .Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naomba na madiwani wa wilaya ya Ilala kuandaa mikutano mikutano ya adhara na Wenyeviti wenu kuelezea mazuri yote yaliofanywa na Rais”alisema Sidde.

Mwenyekiti Sidde alisema kila Diwani wa kata na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa waliotokana na chama cha Mapinduzi CCM wana wajibu wa kuelezea utekelezaji wa Ilani katika mikutano yao adhara watakayoandaa .

Akizungumzia maendeleo ya kata ya Pugu Mwenyekiti Sidde ,alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,Mbunge wa jimbo la Ukonga Jery Silaa na Diwani wa Kata hiyo Imelda Samjela utekelezaji wa Ilani vizuri katika miradi mikubwa ya maendeleo.

Sidde alisema miaka minne ccm iliomba ridhaa wakati wa kuomba kura hivyo ccm aina budi kusimamia na kutekeleza maendeleo ya wananchi kwani ccm imefanya makubwa jimbo la ukonga na kuwataka viongozi walipo madarakani kutatua kero za wananchi.

Akizungumzia Suala la kurasimisha ardhi kata ya Pugu Mwenyekiti Sidde alisema atazungumza na Mbunge wa Jimbo hilo Jerry Silaa ,ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya utatuzi wake.

Akizumzia kero ya Dampo la Pugu CCM wilaya ya Ilala walifanya ziara wamejionea kero hiyo na sasa inaenda kutatuliwa ambapo alisema Dampo la Pugu kwa sasa linaenda kubinausishwa na kila wilaya itakuwa na dampo lao .

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Sidde alisema sakata la mpaka wa Mgeule na Kimani atamleta Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji Jamary Mrisho Satura na wataalam wake kwa ajili ya utatuzi kuhusiana na mpaka wa Kisarawe na Kazimzumbwi pia kero hiyo watawasilisha kwa ajili ya utatuzi wake.

Katibu wa CCM wilaya ya Ilala Frantha Katumwa alimpongeza Diwani Imeda Samjela kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Pugu FRANK MANGATI alisema CCM Kata ya Pugu wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watasimamia miradi yote ya maendeleo inayoelekezwa na Serikali katika kata ya pugu na kuelezea Ilani kwa wananchi wake.

Mwenyekti FRANK MANGATI alisema kata ya Pugu wanajivunia mambo mazuri yamefanywa na Serikali ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu zote ni juhudi za Serikali kwa Kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Ukonga na Diwani wa Pugu

Matukio mbalimbali katika picha