December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM Ilala yawapa rungu wanachama

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

CHAMA cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kimewapa RUNGU WANACHAMA wake wa chama hicho wachague mtu wanayomtaka katika chaguzi za kura za maoni kisha wawasilishe mapendekezo yao ya vikao.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Al haj, said Sidde, wakati wa hafla Maalum iliyoandaliwa na CCM kata ya Ilala ya kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Wilaya .

” Katika chaguzi zozote zitakazofanyika mtafanya uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama mchague mtu mnayotaka halafu mtamuuza wenyewe Ili chama kiweze kushinda chama Cha Mapinduzi akiingili kubadilisha mtu ” alisema Sidde .

Aliwaasa viongozi wa chama cha Mapinduzi kujenga chama na Jumuiya kwani chama cha Mapinduzi kina kazi kubwa katika kusaka Dola 2024 na 2025 katika UCHAGUZI Mkuu .

Aidha katika upande mwingine amewataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa kufanya vikao katika mitaa yao ikiwemo kutatua kero za wananchi na utekekezaji wa Ilani vizuri na muda ukifika wa kutetea Dola wsnachama na WANANCHI wawe na Imani nao watakapotetea nafasi zao .

Akizungumzia CCM kata ya ILALA amewapongeza kwa kuandaliwa hafla fupi keki Maalum na wana CCM wa Kata ya Ilala ni mfano wa kuigwa anawashukuru Ilala kwa kimpatia ushindi mnono wa nafasi hiyo .

Alisema Siasa ameanza mwaka 1989 miaka 12 alikuwa Katibu kata ya Ilala hivyo Ilala yeye ni nyumbani ,baada kutoka Katibu kata Ilala akagombea nafasi ya Siasa na uenezi ambayo amekaa madarakani zaidi ya miaka Kumi .

Alisema CCM inathamini kila mtu Katika mapito yetu CCM na wanachama wa Kata ya Ilala nawaomba Vijana na Wazee mshirikiane katika kujenga chama na kuongoza kata ya Ilala ambayo inatazamwa na kila mtu na inajivunia mafanikio makubwa kwa kutoa viongozi mbalimbali wa Wilaya na ngazi ya Taifa .

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Al haj Said Sidde akikabidhiwa keki maalum iliyoandaliwa na chama Cha Mapinduzi kata ya Ilala Kwa ajili ya kumpongeza Sidde kwa ushindi mkubwa nafasi ya Mwenyekiti (Kushoto anayekabidhi keki )Katibu kata ya ILALA Devotha Bantulaki na (katikati )Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ilala Habibu Nasser (Picha na Heri Shaaban)
Mwenyekiti wa CCM kata ya ILALA Habibu Nasser akisungumza na Viongozi wa CCM Wilaya ya ILALA na Viongozi wa kata ya ILALA wakati wa hafla Maalum ya kumpongeza Mwenyekiti wa Wilaya Said Sidde (Picha na Heri Shaaban )
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya ILALA Said Sidde akizingumza na Viongozi wa chama kata ya ILALA (Picha na Heri Shaban)