November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM :Balozi Nchimbi akukimbia Mdahalo wala kudharau

Na Penina Malundo,Timesmajira 

CHAMA cha Mapinduzi (CCM),kimesema kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi hakukimbia wala kudharau mdahalo wa Makati wakuu wa Vyama mbalimbali ulioandaliwa na moja ya kituo cha Televisheni Agosti 31,2024.

Taarifa iliyotolewa kwa umma leo,ilisema Balozi Nchimbi alifanya kila jitihada za mawasiliano na muandaaji lakini wanasikitishwa na upotoshaji uliofanywa kwa umma.

Imesema Agosti 10, 2024 Mtangazaji wa Kituo hicho cha Televisheni, Edwin Odemba alimtafuta Katibu Mkuu huyo kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (sms)

akimuomba Katibu Mkuu ashiriki mdahalo huo wa viongozi wa vyama vya

siasa uliopangwa kufanyika Jumamosi, Agosti 31,2024.

“Katibu Mkuu alimjulisha kuwa masuala ya vyombo vya habari yanaratibiwa na Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Gabriel Makalla hivyo awasiliane naye na akampa namba ya simu ya mkononi ya Makalla,”imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Imesema kwa sababu ambazo Odemba anaweza kuzieleza mwenyewe, katika kipindi cha takriban wiki tatu, hakufanya mawasiliano au kumtafuta,Makalla kama alivyoelekezwa na kushauriwa na Katibu Mkuu Balozi Nchimbi.

Imesema baada ya kuhisi kwamba nafasi ya Katibu Mkuu inaweza kuwa ngumu

kupatikana kutokana na majukumu yake ya kazi za chama,Odemba alimtafuta tena Balozi Nchimbi akiomba amuandae mwakilishi huku matangazo ya mdahalo huo yakiendelea kumtaja Katibu Mkuu wa CCM kuwa ndiye atakayeshiriki. 

Ilisema kuwa badala yake Katibu Mkuu alimwelekeza Odemba kutofanya lolote kabla ya kupata mawasiliano na Sekretarieti ya Chama.”Kimsingi Odemba alitaka wananchi wadanganywe kuwa CCM kupitia

kwa Katibu Mkuu ilikuwa imethibitisha kushiriki katika mdahalo huo jambo ambalo si sahihi,” imeeleza  na kuongeza

“Katika mazingira ya kustajabisha tumeshangazwa na machozi ya Odemba aliyotoa juzi akielekeza lawama kwa CCM na kwa Katibu Mkuu

wakati alijua bayana kwamba alikuwa hajapata uthibitisho wowote wa CCM

kushiriki ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba yeye mwenyewe alishajua

kwamba alikuwa akiendelea kutangaza kuhusu mdahalo huo kama “promo”

pasipo kupata ridhaa ya CCM,”imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha imesema Katibu Mkuu wa CCM ndiye Mwenyekiti wa Sekretarieti na siku nzima ya juzi ambayo ndiyo siku ya Mdahalo uliopangwa kufanyika kulikuwa

na vikao vya mandalizi ya Kamati Kuu Maalum ambayo imefanyika September mosi 2024.

Imesema jambo ambalo kwa namna yoyote Katibu Mkuu asingeweza kuwapo katika mdahalo huo hata kama angekuwa amethibitisha awali.

“Kushiriki kwenye mdahalo kunahitaji mashauriano na maafikiano kati ya waandaji na waalikwa,tunaweza kutamka bayana na kwa hakika kwamba Katibu Mkuu hakuwa ametoa uthibitisho wa kuhudhuria mdahalo huo.

” Hakukuwa na makubaliano

yoyote rasmi ya yeye au mwakilishi wake kuhudhuria katika shughuli hiyo ,hivyo Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Nchimbi yupo tayari kwa midahalo,

majadiliano na makongamano yanayolenga kujenga umoja wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa kadiri ya taratibu zilizopo na ratiba yake ya kazi inavyoruhusu,”imesisitiza taarifa hiyo.