Mwandishi wetu, TimesMajira Online
CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE) kimewakaribisha wananchi wote wenye sifa na vigezo kuomba nafasi za masomo katika chuo hicho .
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo hicho (CBE) Profesa Tandi Luoga wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.
Amesema chuo hicho kina kozi nyingi kwa ngazi mbalimbali zikiwemo za mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ambapo katika mafunzo ya muda mrefu wanaotoa elimu kuanzia ngazi ya cheti ,diploma,bachelor na masters .
Profesa Luoga amesema Kwa chuo hicho kwa sasa kimekuja kivingine kwani kimeanza kutoa masters kwa njia mtandao.
“Kwa sasa tuna wanafunzi wanaoshiriki masomo kwa njia ya mtandao ambapo mahali popote walipo wanapata masomo yao .”amesema
Na kuongeza kuwa
“Kupitia programu hii inakwenda kumrahisishia mtumishi kusoma bila kuathiri shughuli zake programu hii mtandaoni imeanza Machi mwaka huu huu huku akisema hii ni kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia katika kurahisisha mambo”amesema Profesa Luoga
Aidha amesema Chuo hicho chenye matawi manne katika mikoa ya Dar Es Salaam ,Dodoma,Mwanza na Mbeya kimefikia maamuzi huo wa masomo mtandaoni ili kutoa wigo mpana hasa kwa watumishi na makundi mengine kujiendeleza kielimu.
Amesema mwanafunzi wa Masters anayesoma kwa njia ya mtandao , hahitaji kwenda mpaka CBE Mwanza,Dodoma Mbeya au Dar Es Salaam kusoma isipokuwa wakati wa mitihani ambapo mwanafunzi anaenda kwenye Tawi lolote la chuo hicho lililo karibu naye.
“Hatua hii imesaidia kusambaza elimu ya biashara ndani na nje ya Tanzania, lakini imepunguza gharama kusafiri na malazi kwa mwanafunzi husika.”amesisitiza
Aidha amesema chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya muda mfupi mfupi kwa wajasiliamari na wafanya biashara ambapo katika mafunzo hayo tunasamabaza matokeo ya tafiti ili waweze kuyaelewa na kuyatumia
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa