March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bulugu awahamasisha vijana wa Mlowo kuichagua CCM

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa CCM, Bulugu Magege, amekutana na vijana wa Kata ya Mlowo na kuwasisitiza kuhakikisha kura zao zote wanampa Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wa CCM katika ngazi zote.

Katika mazungumzo hayo, Bulugu amewaeleza vijana kuwa Ilani ya CCM imewapa kipaumbele kikubwa vijana ikiwemo mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, ajira, elimu bora na uwezeshaji kiuchumi.

Amesisitiza kuwa Dkt. Samia ni Rais mwenye upendo mkubwa kwa vijana, anayetamani kuwaona wakibadilisha maisha yao kupitia fursa alizozileta.

Bulugu aliambatana na Haji Shabani Mwalimu, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbozi na Noel Donald Mkwemba, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Mkoa wa Songwe. Vijana wa Mlowo walimhakikishia kuwa wako tayari kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo ifikapo Oktoba 29, 2025.