Na Esther Macha Timesmajira Online,Mbeya
WAKULIMA kutoka mikoa mbalimbali nchini wametakiwa kurasimisha biashara pamoja na kuanzisha makampuni kwa kuzingatia kanuni na taratibu za Wakala wa Usajili na Leseni (BRELA).
Akizungumza na Timesmajira,Mkuu wa kitengo cha uhusiano wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA),Roida Andusamile amesema kuwa wapo katika viwanja vya Maonesho ya wakulima Nanenane ambayo yanafanyika kimataifa mkoani Mbeya kwa lengo la kutoa elimu kwa wakulima na wadau wengine.
“BRELA ni wadau wa maonyesho haya ya wakulima kwa maana kwamba tunawezesha biashara,kwanini tunasema kilimo ni biashara kama kilimo ni biashara wanapaswa kurasimisha biashara zao maana mkulima haishii kulima tu anauza mazao pia kwa hiyo anatakiwa kurasimisha biashara ndo maana tupo hapa kuhamasisha kutoa elimu ili waweze kurasimisha biashara zao “amesema
Aidha Andusamile amesema kuwa wanaposema kurasimisha biashara ni pamoja na kusajili majina ya.biashara, Kampuni, alama za biashara na huduma, kupata leseni za biashara kundi A ,viwanda na kusajili viwanda vidogo na kwamba zote zinatolewa.
Amesema kwamba katika Maonesho hayo ya wakulima wanatoa huduma za papo kwa hapo na wadau na wakulima wanajitokeza wanasajili majina ya biashara ,kampuni na utaratibu wa BRELA wanatumia kwa njia ya mfumo kuna wengine wanapata changamoto katika usajili na ndo sababu wanafika katika bando hilo kupata usaidizi na wengi wanaokamilisha taratibu zote wanaondoka na vyeti.
“Mbali na sisi kutoa huduma katika mabanda yetu bado tumekuwa tukipita kwenye mabanda ya wakulima na kutoa elimu ya kurasimisha biashara zao na kama hawana elimu tunatoa kwa hiyo Maonesho haya kwetu ni fursa kubwa kama BRELA kujitangaza pia kutoa elimu kwa wadau kutoka mikoa mbalimbali nchini kuwahudumia watu wote hawa ni fursa kubwa kwetu “amesema Ofisa uhusiano huyo.
Hata hivyo Andusamile ametoa wito kwa wafanyabiashara ,wadau, wakulima wafike katika mabanda ya BRELA ili kuweza kupata huduma ya urasilimishiji wa biashara zao na kwamba hiyo Taasisi wapo kuhudumia wananchi na hawapo kibiashara.
Akizungumzia kuhusu mwitikio wa wananchi Andusamile amesema kuwa ni mzuri kwani mpaka sasa wameweza kutembelewa na wadau zaidi ya 104,ambao wanaendelea kujitokeza kupata elimu na kwamba wana Imani mpaka mwisho wa maonesho ya watakuwa wamehudumia watu wengi zaidi.
Mmoja wa Wananchi waliofika katika Maonesho hayo,Atuganile Mwakyusa amesema yeye Kama mkulima amefurahishwa na huduma hizo kwani amepata vitu vingi zaidi ambavyo alikuwa havifahamu kuhusu Brela.
“Elimu hii niliyopata nitaenda kuwa barozi mzuri kwa wakulima wenzangu ambao hawana elimu hii maana wengi wetu tulikuwa tunajifanyia tu biashara zetu bila kusajili ” amesema mkulima huyo.
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi