Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa mwito kwa wafanyabiashara nchini kulinda alama zao za biashara sambamba na kulinda bidhaa zinazozalishwa nchini na kwa kufanya hivyo watakuwa wamelinda uchumi wa nchi yao.
Akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandalwa na wakala huyo iliyofanyika leo Januari 19, 2022 Jijini Dar es Salaam iliyolenga kuwajengea uelewa wafanyabiashara hao, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya miliki ubunifu wa BRELA Bwa. Seka Kasera, sema kuwa endapo wafanyabiashara wataelimika katika kulinda bidhaa zinazozalishwa nchini watakuwa wamelinda uchumi wa Taifa.
“Unapolinda bidhaa zinazozalishwa nchini unalinda uchumi wa Taif, hivyo wafanyabiasha wanapaswa kutumia na kuzilinda alama zao za Biashara” amesema Kasera.
Ameongeza ili nchi iweze kusonga mbele ni lazima technojia itumike hasa kulinda alama zao (Logo) itakayo wawezesha kulinda bidhaa zao na kupunguza migogoro ya kuiga alama ya mtu mwingine.
“Kuna wengine hawazipi kipaumbele alama zao za biashara hivyo kwa kongamamo hili wafanyabiasha watapata mafunzo ili wazipe kipaumbele ‘Logo’ zao”
Ameongeza kuwa anaamini mafunzo hayo yatakwenda kuwaongezea uwezo katika uzalishaji wa bora na zenye viwango vya kimataifa na kwamba mafunzo hayo yatasambazwa nchi nzima.
“Mafunzo haya yatasambazwa nchi nzima hasa kwa Wafanyabiasha wadogo wadogo ili wote waweze kupata mafanikio kwenye soko la kimataifa na kuweza kuongeza thamani katika bidhaa zao” amesema Bw. Kasera.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Martin Mbwana na Agripina Thomas wameishukuru BRELA kwa kuwapatia mafunzo hayo na kwamba wanaamini elimu hiyo itawawezesha kuzalisha bidhaa zenye ubora zaidi.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato