Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online Dkt Ashatu Kijaji, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara akipata maelezo juu ya huduma tunazozitoa kwenye maonesho ya tisa ya biashara na utalii kutoka kwa Afisa Leseni Bi Saada Kilabula. Maonesho haya yameanza tarehe 28 Mei, 2022 mkoani Tanga. Dkt Hashil Abdallah, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, akipata maelezo ya namna Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inavyotoa huduma zake kwenye maonesho ya tisa ya biashara na utalii yanayoendelea mkoani Tanga kuanzia tarehe 28 Juni, 2022 Afisa Tehama Msaidizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Hillary Mwenda akitoa usaidizi wa usajili wa Jina la Biashara kupitia mfumo wa usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) kwa Bw. Emmanuel Mallya kutoka Korogwe-Tanga kwenye Maonesho ya Tisa (9) ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Uwanja wa Mwahako mkoani Tanga. Katika maonesho hayo BRELA pia inatoa huduma za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, kupata Leseni ya Kiwanda, Leseni ya Biashara kundi A, kupata Hataza na kutoa mafunzo pamoja na usaidizi juu ya kutumia mfumo wa ORS. Afisa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Julieth Kiwelu akitoa elimu ya Hataza kwa Bw. Musini Abdallah katika Maonesho ya Tisa (9) ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Uwanja wa Mwahako mkoani Tanga. Katika maonesho hayo BRELA pia inatoa huduma za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, kupata Leseni ya Kiwanda Leseni ya Biashara kundi A, na mafunzo pamoja na usaidizi juu ya matumizi ya mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS). Msajili Msaidizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Selemani Selemani akitoa usaidizi kwa Bi. Hafsa Kwallow juu ya namna ya kujaza katiba ya kampuni kwenye Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) kwenye Maonesho ya Tisa (9) ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Uwanja wa Mwahako mkoani Tanga hadi tarehe 6 Juni, 2022. Katika maonesho hayo BRELA inatoa huduma za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, kupata Leseni ya Kiwanda, Leseni ya Biashara Kundi A, kupata Hataza na kutoa mafunzo na usaidizi juu ya matumizi ya mfumo wa ORS. Post Views: 350 Continue Reading Previous Viongozi wa Kimila Tarafa za Loliondo na Ngorongoro wawasilisha ripoti maalumNext Halmashauri zatakiwa kutenga pesa za mikopo kwa vikundi vya waviu More Stories Habari CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa November 6, 2024 Penina Malundo Habari CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa November 6, 2024 reuben kagaruki Habari Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba November 6, 2024 reuben kagaruki
More Stories
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba