Na Mwajabu Kigaza, Kigoma
WATU 10 wamekufa kutokana na ajali ya boti iliyozama katika Ziwa Tanganyika kwenye eneo la kambi ya wavuvi makakara Kijiji cha Rufugu wilaya ya Uvinza Mkoani kigoma .
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma ACP, James Manyama alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Akizingumza kwa njia ya simu jana alisema kuwa taarifa za awali zinaeleza kuwa watu sita wamekufa huku idadi kamili ya abiria waliokuwa katika boti hiyo haijulikani.
Baadhi ya mashuhuda na wakazi wa eneo hilo wakizungumza kwa njia ya simu akiwemo Juma Yakuti na Kaliya Kazibure wameeleza kuwa tukio hilo limetokea saa nne asubuhi ambapo boti hiyo lilikuwa likitoka Kijiji cha Sibwesa kuelekea Ikora mkoani Katavi.
Walisema chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na boti waliyopanda abiria hao kujaza watu kupita uwezo wa boti hiyo na hivyo kusababisha kuzama majini.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ameeleza kuwa taarifa zaidi juu ya tukio hilo zitaendelea kutolewa. Mwezi mmoja iliopita ajali kama hii ilitokea katika eneo la kijiji cha Simbwesa ambapo watu tisa walifariki kati ya abiria 60 waliokuwemo katika boti.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati