Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Nishati January Makamba amesema bomba la TAZAMA lenye urefu wa Km 1,710 kutoka Kigamboni-Dar es Salaam hadi Ndola-Zambia linatarajiwa kupanuliwa ili kukidhi mahitaji ya mafuta katika soko la Zambia na baadhi ya mikoa ya Tanzania.
Waziri Makamba aliyasema hayo jijini DSM wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika kikao Cha Mawaziri sita wa Tanzania na Zambia.
Waziri Makamba Alisema miradi hiyo ni mikubwa na muhimu ya kimkakati nchini kwasababu bomba hilo la TAZAMA linasafirisha lita milioni 90 za mafuta ya Dizeli kwa mwezi .
“Tukijenga bomba kubwa zaidi Bandari itapata soko kubwa kwa mafuta yanayoenda Zambia na Kongo, lakini pia itasaidia mikoa ya kusini mwa Tanzania kupata mafuta kwa unafuu kwasababu kwenye bomba jipya kutakuwa na matoleo ya kushusha mafuta katika mikoa ya morogoro, Iringa, Mbeya na Songwe”
“Barabarani kutakuwa na magari machache zaidi na gharama za usafirishaji zitakuwa chini zaidi ndiyo maana kikao hiki ni muhimu”.
Kikao hicho Cha pili kilichofanyika jijini DSM kimejumuisha waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni, Waziri wa Ulinzi, Innocent Bashungwa.
Kwa upande wa Zambia walioshiriki ni pamoja na Lufuma, waziri wa mambo ya ndani, jack Mwiimbu na Waziri wa Nishati , Peter Kapala.
Kikao hicho Cha Mawaziri kilitanguliwa na kikao Cha makatibu Wakuu wa wizara pamoja na wataalamu kuhusu taratibu za kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta na bomba la gesi asilia.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Zambia Ambrose Lufuma alisema ndege ndogo zisizo na Rubani (drone) zinatarajiwa kutumika katika ulinzi wa bomba la mafuta linalotumika kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Dar es Salaam -Tanzania Hadi Ndola – Zambia .
Aidha alisema mbali na drone, pia wanakijiji ambao bomba hilo lililojengwa miaka ya 1970 linapita, wanatarajiwa kushirikishwa kikamilifu katika ulinzi wa bomba hilo ambalo tangu January mwaja huu linasafirisha mafuta ya Dizeli badala ya mafuta ghafi ambayo yalipigwa marufuku na serikali ya Tanzania .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba