Na David John timesmajiraonline
RAIS Wa Shirikisho la Wachimba Madini Tanzania FEMATA John Bina amempongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuendelea kutengeneza mazingira wezeshi kwa wawekezaji wanaokuja hasa katika sekta ya madini.
Bina ametoa kauli hiyo leo Juni 6 katika viwanja vya maonyesho ya 46 ya kimataifa ya sabasaba wakati akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutembelea mabanda ya madini yaliyo chini ya shirika la madini la taifa STAMICO
Pamoja na mambo mengine amelisifu shirika hilo la taifa la madini kwakuweza kuwaleta pamoja wa wadau wa madini kupitia maonyesho hayo nakwamba dunia ujuwe kuwa Tanzania yanachimbwa madini.
” hapa nataka niseme nakuwaomba ninyi waandishi kuandika vizuri kwa kutumia karamu zenu na kamera zenu ili kuifanye sekta ya madini hasa wageni wajuwe Tanzania yanachimbwa madini na wao tunawakaribisha. “amesema
Nakuongeza ” Mh. Rais anafanya kazi nzuri sana ya kukaribisha wawekezaji lakini kikubwa lazima hapa niseme kwamba tunahitaji asilimia hamsini kwa hamsini.
Pia rais huyo wa Shirikisho amefafanua kuwa Hayati Magufuli alitoa ruksa ya kuchimba madini changamoto ilikuwa wanachimbaji nakukiri kwamba alifanya kazi nzuri sana nakwamba hivi sasa Mama mh Rais Samia anatengeneza mazingira wezeshi ilikuweza kuchimba madini.
” Hivyo leo nimekuja hapa sabasaba niseme nimefurahi sana na hasa katika. Mabanda yeti ya shirika hili la Madini Stamico kwakuweza kuwakusanya pamoja wachimbaji. “amesisitiza Bina
Kiongozi huyo pia ameongozana na viongozi mbalimbali wa Shirikisho hilo akiwamo katibu mkuu lister Festo Makamu Mwenyekiti wajumbe na wadau wengine kutoka Shirikisho la madini Tanzania.
More Stories
Serikali kuwezesha CBE kuwa kituo mahiri
TCC yaibuka kidedea tuzo za PMAYA
Mwanafunzi apoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba